Daily Archives: October 10, 2019

ZRB YATEKELEZA AZIMIO LA KUIMARISHA USTAWI WA MTOTO

Katika kutimiza maazimio ya mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu kuimarisha ustawi wa mtoto bodi ya mapato Zanzibar ZRB imetekeleza azimio hilo kwa kutoa msaada wa magodoro na vitabu katika kituo cha kulelea watoto yatima mazizini ikiwa ni kutimiza ahadi waliyoitoa kwa kituo hicho.

Akikabidhi msaada huo mwenyekiti wa bodi ya ZRB Nd. Saleh Osman Sadiq amesema ZRB kutokana na uundwaji wake inasaidia changamoto nyingi zinazowakabili wananchi hivyo imetoa msaada huo ili kuona watoto hao wanalelewa katika mazingira ya kuridhisha.

Naibu katibu Mkuu wizara ya kazi, uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto Nd. Mwanajuma Majid amesisitiza bodi hiyo na taasisi nyengine kwa pamoja kuzidisha juhudi za kustawisha maisha ya watoto katika jamii ili kujenga taifa imara litakalokuwa na vijana wenye imani thabiti ya kuipenda nchi na raia wake.

 

WAKALA WA MKONGA ZANZIBAR WATAKIWA KUFANYA KAZI ZAO KWA MUJIBU WA TARATIBU ZA SERIKALI

Waziri wa ujenzi mawasiliano na usafirishaji Mhe Dkt Sira Ubwa Mamboya ameitaka bodi ya ushauri wa wakala wa mkonga zanzibar kufanya kazi zao kwa mujibu wa taratibu za serikali zilizopo.

Mhe Waziri ameyasema hayo alipokuwa akizundua rasmi bodi hiyo huko katika ukumbi wa mikutano wa wizara ya ujenzi kisauni nje kidogo wa mji Zanzibar.

Dkt Sira amesema matumaini yake ni kuwa bodi hiyo itaendelea kumshauri na kupendekeza mambo yanayofaaa kwa manufaa ya umma na kuitaka bodi hiyo kutunza siri pamoja na kufanya kazi kwa uaminifu na uweledi ili kufanikisha malengo yaliyopo.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt Haji Ali Haji ameahidi kuwa watafanya kazi kwa uwaminifu na uweledi mkubwa ili kufikia malengo ya uchumi wa kati, mkuza namba lll pamoja na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kama inavyoagizwa na rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.

Nae mkurugenzi utumishi na uwendeshaji wa wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji ndugu Bimkubwa Abdi Nassib alitoa nasaha zake kwa bodi hiyo kwa kuishauri kufuata miongozo ya kazi zao na kutomuangusha mhe rais  kwa imani waliyopewa.

MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UKATILI KWA WATOTO YAENDELEA

 Waziri wakazi uwezeshaji wazee wanawake na watoto MH Moudeline Cyrus Castico ameitaka jamii kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa watoto.

Castico ameyasema hayowakati akifungua kongamano la kitaifa la kujenga uelewa na kuhamasisha utekelezaji wa sheria za kupambana na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto lililofanyika ukumbi wa ZSSF kariakoo mjini Zanzibar.

Mh Castico amesema nijukumu letu kuhakikisha  kuwa watoto wanalindwa na wanatunzwa ili kuwa na wataalamu na viongozi bora hapo baadae.

Baadhi ya washiriki katika kongamano hilo wameelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na watoto katika jamii na kuitaka serikali  kuchukua hatua nakuhakikisha vitendo vya udhdalilishaji vinatoweka nchini .

Kwa upande wake jeshi lapolisi limeitaka jamii kuachana na vitendo hivyo vya udhalilishaji na kushirikiana na jeshi hilo kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wa vitendo hivyo kwani imekuwa nitatizo kubwa linalo ikumba  nchi kwasasa.

error: Content is protected !!