Daily Archives: October 9, 2019

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE ZANZIBAR INAHAKIKISHA USALAMA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZAKE

Mamlaka  ya  viwanja  vya  ndege  Zanzibar inalenga  kuhahakikisha  kuwa  kupanuka  kwa  huduma  na  ongezeko  la   ndege   katika viwanja  vyake   ni  kunaendana   na   uhakika  wa  usalama  katika  utoaji wa  huduma.

Tamko  hilo  limetolewa  na  meneja  wa  kiwanja  cha ndege  cha kimataifa cha  Abeid  Amani  Karume  wakati  akifungua  mafunzo  juu  ya  usalama   wa  viwanja  vya  ndege kwa  watendaji  wa  idara  mbali  mbali yalioendeshwa  na wakufunzi  kutoka  mamlaka  ya  viwanja  vya  ndege  Tanzania  .

Amesema lengo  ni  kuwatarisha  wafanyakazi  kutambua hatua  za  awali  za  matukio  ya  hatari  katika  viwanja  vya  ndege  na  kuweza  kuchukua  hatua  zinazofaa  na  za  kitaalamu  katika  kuzipatia  ufumbuzi kulingana  na  kanuni  za  kimataifa.

Mkufunzi  Benard  Kavishe kutoka  mamlaka ya  viwanja  vya  ndege  Tanzania  amesema  utoaji  wa  huduma  katika  viwanja  vya  ndege  duniani unakabiliana  na  changamoto tofauti  lakini  zinaweza  kuepukika  iwapo  watoaji  wa  huduma na  wadau   watakuwa  wakijengewa  uelewa  wa  kufahamu  jinsi  ya  kuzitatua.

Uwanja  wa  ndege  wa   Abeid  Amani  Karume  umekuwa  na  ongezeko  la  ndege  zinazotuwa  kufuatia  kuimarika   kwa  huduma  kulikochangiwa  na  ujenzi  wa  bararara  ya  kuruka  na  kutua  kwa  ndege kiwanjani  hapo,

WAFANYA BIASHARA WAIOMBA SERIKALI KUEKA MIUNDOMBINU ITAKAYOWEZESHA KUKUZA KIWANGO CHA BIASHARA

 Wafanya biashara  kisiwani Pemba wameiomba Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, kuimarisha miundombinu itakayowezesha kukuza kiwango cha biashara na kupata mapato mazuri yatakayo saidia kuinua hali ya uchumi  nchini.

Wafanya biashara hao wametoa wito huo wakati walipokuwa wakipatiwa mafanzo juu ya mabadiliko ya sheria za kodi zinazosimamiwa na TRA huko kwenye ukumbi wa maktaba kuu chakechke.

Mapema afisa mdhamini wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa upande wa Pemba, Habaib Saleh Sultan amewataka wafanya biashara kutoa mashirikiano mazuri katika kulipa kodi za serikali.

Akiwasilisha mada ya mabadiko ya sheria za kodi zinazosimamiwa na TRA afisa elimu kwa walipakodi Shuwekha Seif Khalfan akizitaja baadhi ya sheria zilizofanyiwa mabadiliko amasema

WAPANGAJI WA NYUMBA ZA MICHENZANI WAMELISHAURI SHIRIKA LA NYUMBA KUIMARISHA MAZINGIRA YA NYUMBA HIZO

Wapangaji wa nyumba za maendeleo michenzani wamelishauri shirika la nyumba kuimarisha mazingira ya nyumba hizo kutokana na kasi ya mabadiliko ya miji.

Wakizungumza katika mkutano wa kujadili rasimu ya mkataba wa huduma za umma uliofanyika rahaleo wameeleza kuwa kufanyahifo kutasaidia kuimarisha majumba hayo mamoja na kuleta haiba katika mazingira ya mjini.

Mkurugenzi mkuu  wa shirika la nyumba Zanzibar Bi Riziki Jecha Salim amewataka wananchi wanoishi katika nyumba za maendeleo kuzitunza nyumba hizo pamoja na kufuata sheria za shirika la nyumba.

Akiwasilisha mada juu ya mkataba wa huduma kwa umma na mambo mengine yanayohusiana na hayo kaimu mkurugenzi utawala na rasilimali watu kutoka shirika la nyumba Zanzibar Bi Mwantum Ramadhan Mussa amesema wajibu wa mkataba  ni pamoja na kutoa taarifa sahihi na kwa wakati na kutoa huduma bora kwa walengwa.

Washiriki wa mkutano akiwemo sheha wa shehia ya Rahaleo Bi Mwanakheir Sultan na bwana Mohamed Mugheir wameomba watendaji wa shirika hilo kutoa taarifa kwa masheha pindi wanapotoa mikataba kwa wapangaji ili kuepusha usumbufu.

 

error: Content is protected !!