Daily Archives: October 8, 2019

SMZ KUKIFUFUA KIWANDA CHA KUTENGENEZEA NGUO KILICHOPO CHUMBUNI

Serikali ya mapinduzi Zanzibar  imesema itaendelea   kukifufua  kiwanda cha kutengenezea  nguo  kilichopo chumbuni ili kukirejesha kiwanda hicho kufanya kazi kama kawaida .

Akizungumza na zbc waziri wa biashara na viwanda  Balozi Amina Salum Ali  amesema sera ya serikali ni kuanzisha viwanda ili vijana  wapate  ajira na kuinua uchumi wa nchi.

Amesema  kiwanda  hicho kimekaa  muda mrefu hakifanyi kazi  na sasa hivi tayari wameshawakabidhi kampuni ya basra kutoka kenya  kukisafisha kwa kutia  dawa  ili kutoa sumu zilizokuwemo .

Aidha Balozi Amina amesema wameshafanya utafiti wa kiasi cha maji na umeme utakaoweza kutumika katika maeneo ya kiwanda hicho  na wiki ijayo tarifa zote zitakuwa tayari

PBZ YAJIPANGA KILA MWANANCHI WA TANZANIA APATE HUDUMA BORA KUTOKA KWAO

Benki ya watu wa ZanzibarPBZ imesema imejipanga kuhakikisha kila mwananchi wa Tanzania anapata huduma bora zinazotolewa na benki hiyo kulingana na mahitaji yake kutoka  benki hiyo.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na mkurugenzi mtendaji wa PBZ Juma Ahmed Hafidhi ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo amesema kwa sasa inaendelea na kuimarisha huduma zake ikiwemo kuongeza matawi katika mikoa ya tanzania bara

Nae kaimu meneja PBZ tawi la kariakoo jijini Dar es salaam Yusufu Ramadhani amesema kutoka na kuimarisha kwa mfumo wa kibenki imesaidi kuanzishwa kwa huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya PBZ sim benki na huduma ya kutuma pesa nje ya Nchi.

Kwa upande wao baadhi ya wateja benki hiyo wamesema ubora wa huduma zinazotokewa na PBZ ndio miongoni mwa sababu zilizowapelekea kufungua akaunti katika benki hiyo.

Katika kuadhimisho wiki ya huduma kwa mteja benki ya pbz imetoa zawadi kwa wateja wake ikiwa ni sehemu ya kurejesha faida waliyoipata.

error: Content is protected !!