Daily Archives: October 7, 2019

WAZEE WAMESHAURIWA KUJIHUSISHA NA MICHEZO PAMOJA NA MAZOEZI YA VIUNGO

Wazee wameshauriwa  kujihusisha na michezo  pamoja na mazoezi ya viungo  ili kuimarisha afya zao .

Akizungumza katika bonanza  la michezo  mbalimbali lilofanywa na wazee  kutoka  mkoa wa kaskazini,  kusini   na mkoa wa mjini magharibikatika kuadhimisha siku ya wazee duniani,naibu wa ziri wa kazi,uwezeshaji,wazee,wanawake na watoto ,Shadya Mohamed Said amesema kuwa  wakati umefika sasa kwa wazee  kushiriki katika michezo tofauti kwa  ili kujijenga kiafya na kuondokana na matatizo mbalimbali  yanayoweza kujitokeza mwilini yakiafya.

Mkurugenzi wa kituo cha kuwaenzi na kuwalinda wazeecha mkoa wa mjini magharib ,Ameir Ali Ameir amesema kuwa licha ya kuwa wanaadhimisha siku ya wazee duniani, lakini lengo hasa la kuandaa bonanza hilo kuwaonesha wazee jinsi gani wanathaminiwa na pia kuwapa fursa ya kujuana na kushirikiana katika harakati mbalimbali za kijamii.

Miongoni mwa michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni pamoja na mpira wa miguu,mchezo wa bao,karata,kuvuta kamba  na mchezo wa kufukuza kuku.

Kwa upande wa wazee walioshiriki na waliojionea bonanza hilo wamsema kluwa  wamefarijika kukutana  kwa pamoja leo na wanajisikia bado wanathamani kubwa katika jamii.

 

 

 

WAKULIMA WAMEIOMBA WIZARA YA KILIMO KUWASAIDIA KUPATA DAWA ZA KUONDOSHA MARADHI KWA KILIMO CHAO

Wakulima wanaolima mboga mboga katika eneo la migombani jeshini  wameiomba wizara ya kilimo kuwasaidia kupata dawa  itakayosaidia kuondosha maradhi  yanayoharibu kilimo chao.

Wakizungumza na zbc  wakulima hao wamesema wamekuwa wakitumia nguvu nyingi katika kilimo hicho lakini mafanikio wanayoyapata ni madogo kutokana na mboga zao  kunyauka kabla ya kufika wakati wa kuvuna.

Wamesema tatizo hilo ni la muda mrefu  na ufumbuzi wake hawajaupata  licha ya jitihada wanazozichukuwa  za kutafuta wataalam.

Wakati huo huo akina mama wanaojishughulisha na ufugaji wa kuku katika shehia ya mtende wilaya kusini unguja  wamesema  wizi wa kuibiwa mifugo yao unawafanya kutofikia malengo waliyojipangia.

Naibu sheha wa shehia ya mtende  amethibitisha kuwepo kwa wizi huo na kusema  katika kupambanda na tabia hiyo imeanzishwa kamati ya ulinzi na usalama ili kuhakikisha inakomesha vitendo hivyo sambamaba na  uovu mwengine wowote.

 

VIJANA WANA PASWA KUZITUMIA FURSA ZILIZOPO KATIKA KUYAPATIA UFUMBUZI MATATIZO YANAYOWAKABILI

Mwenyekiti   wa  umoja  wa  watu wenye ulemavu  Zanzibar ndugu Salma Haji Saadati  amesema vijana wana paswa kuzitumia fursa zilizopo katika kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili.

Akizungumza  katika  mafunzo ya stadi za  maisha   na umiliki wa  rasilimali  kwa vijana   amesema ni vyema  taaluma  wanazopatiwa  vijana   kuzitumia  kwa  lengo  la  kujikwamua  na  ukosefu  wa  ajira.

Amesema  baadhi ya vijana wanashindwa  kujitambua  na kusababisha  kujiingiza katika  matukio mabaya ikwemo ubakaji na udhalilishaji licha ya kuwa zipo fursa nyingi za kujijengea maisha yao .

Akitoa  mada ya  ulemavu  na haki za  binadamu, kaimu mkurugenzi   wa  umoja wa   watu wenye ulemavu nd  mohd abdallah  mohamed  amesema ulemavu ni sehemu ya pili  ya  maisha  ya  mwanadanu hivyo jamii  inapaswa kubadili mtazamo na kuutanguliza utu  kwanza.

akifungua mafunzo hayo mratibu  wa mradi wa kuwawezesha vijana  kiuchumi  hababuu  makame  gharibu  amesema lengo  la mafunzo hayo ni  kuweka usawa  kwa watu wenye ulemavu  na   kuwajengea uwezo wa kujiunga na vikundi vya ujasiri amali

error: Content is protected !!