Monthly Archives: September 2019

DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEREJEA NCHINI AKITOKEA NCHI ZA UMOJA WA FALME ZA KIARABU UAE

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amerejea nchini  akitokea nchi za umoja wa falme za kiarabu uae kwa ziara ya wiki moja ambapo amefanya ziara nchini ras al khaimah pamoja na abudhabi ikiwa ni mualiko wa kiongozi wa ras al khaimah sheikh saud bin saqr al qasimi

Ziara hiyo ya Rais Dk. Shein ilianza tarehe 23 na kumaliza jana tarehe 28 Septemba mwaka huu 2019 ambapo katika ziara hiyo, alipata fursa ya kuzungumza na mwenyeji wake Mtawala wa Ras-Al-Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi pamoja na kuzungumza na Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Rais Dk. Shein alipokewa na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali pamaaoja na  viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.

Mara baada kuwasili kiwanjani hapo, Rais Dk. Shein alifanya mazungumzo na Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vikiwemo vya Serikali na binafsi ambapo katika maelezo yake alieleza mafanikio makubwa ya ziara hiyo ikiwa ni pamoja na mapokezi mazuri aliyoyapata yeye na ujumbe wake aliofuatana nao.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza hatua zilizofikiwa na Kampuni ya Mafuta ya “RAK GAS” inayojishughulisha na utafiti wa mafuta na gesi asilia hapa Zanzibar na kusisitiza kuwa kazi iliyofikiwa ni nzuri na kila hatua itakayofikia wananchi wataelezwa.

Rais Dk. Shein aliwataka wananchi wasihadaiwe na wale wanaopenda kusema kuwa Rais amefunja sharia na katiba  na kusisitiza kuwa suala la mafuta na gesi liko vizuri wala hakuna Sheria wala Katiba iliyovunjwa.

Rais Dk. Shein pia, alieleza namna ya Kiongozi wa Abudhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan alivyomuhakikishia kuwa yuko tayari kuiunga mkono Zanzibar katika kutafuta nishati mbadala ambayo kwa upande wa Zanzibar nishati hiyo inatazamiwa kuwa itakuwa nishati ya jua.

Alieleza kuwa tayari Zanzibar kazi imeshaanza kufanywa katika kuhakikisha nishati mbadala ya jua ndio kipaumbele ambapo kwa mashirikiano ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na Umoja wa Ulaya (EU).

Pamoja na hayo, Rais Dk. Shein alieleza kuwa tayari kuna wawekezaji ambao wako tayari kuja kuekeza katika umeme wa jua ambapo kwa upande wa Serikali imo katika kuandaa mipango madhubuti.

Rais Dk. Shein alieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa fedha zake wenyewe kwa ajili ya uendeleza wa ujenzi wa jengo jipya la abiria la uwanja wa ndege huku akieleza hatua za ujenzi wa bandari mpya ya Mpigaduri ambayo alieleza azma ya Serikali kuanza ujenzi japo wa awali kabda hajamaliza muda wake.

Alieleza kuwa tayari fedha za Mkopo kutoka Benki ya Exim ya Indonesia umepatikana sambamba na ujenzi wa bandari ya mafuta na gesi huko Mangapwani ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kwa upande wa msaada wa fedha Bilioni 23 zilizotolewa na Mfuko wa Khalifa Fund, Rais Dk. Shein alisema kuwa mbali ya fedha hizo pia, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wake itatoa fedha kama hizo na kufikia Bilioni 46 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wakiwemo wajisiriamali na wanawake

Alisisitiza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano na ushsirikiano kati ya wafanyabiashara wa Zanzibar na wale wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Akiwa UAE, Rais Dk. Shein alikutana na viongozi mbali mbali wakiwemo wa Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na gesi asilia ya Ras Al Khaimah “Rak Gas”, Kampuni ya RAKEZ, Kampuni ya Mji wa Bahari wa Ras Al Khaiman, Mamlaka ya Uendelezaji Utalii ya Ras Al Khaimah, uongozi wa Taasisi ya Sera na Utafiti ya Kiongozi wa Ras Al Khaiman.

WANANCHI WAMETAKIWA KUTUNZA NA KUENZI UTAMADUNI

Wananchi wametakiwa kutunza utamaduni  na kuenzi  kwani ndio unaokusanya na kuleta  vivutio mbalimbali   vya utalii ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika ufungaji wa tamsha la mtanzania  katika ukumbi wa ngome kpngwe Mh Naibu Waziri wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji Mh Mohammed Ahmada Salim amesema  matamasha kama haya yanakuza utalii ikiwemo na utamaduni  ndio unaokusanya watu mbalimbali na vivutio viliopo ndani ya z’bar .

Hata hivyo amesisitiza kuwa utalii ni uti wa mgongo katika visiwa vya z’bar  kwani kiasi cha shilingi milioni 5 zimeweza  kupokelewa kutokana na utalii.

Tamasha hilo la pili ambalo  limepambwa kikundi cha modem taarab,pamoja na michezo mbalimbali ya bao na mchezo wa draft. Ambayo ilisisimua hisia za wananchi waliofika katika eneo hilo.

WANANCHI WAMETAKIWA KUITHAMINI MIRADI YA MAENDELEO INAYOFIKISHWA NDANI YA MAJIMBO

Wakaazi wa shehia ya mnarani jimbo la Pangawe  wametakiwa  kuithamini miradi ya maendeleo inayofikishwa ndani ya jimbo lao ile iweze kudumu kwa muda mrefu na kuwaletea tija kwa ajili ya maendeleo yao na vizazi vijavyo.

Mwakilishi wa jimbo la Pangawe Mh Khamis Juma Maalim  amesema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa kisima cha  maji safi  na salama  kwa ajili ya wananchi wa  maeneo ya angaza mnarani  kilichofadhiliwa na shirika la direct aid Zanzibar.

Amewaahidi wananchi hao kuwa wataendelea kushughulikia matatizo mbalimbali yanayowakabili na kurudisha nyuma mandeleo yao

Diwani wa kuteuliwa  wilaya ya magharibi b  Thuwaiba Jeni Pandu amesema eneo hilo  lilikosa huduma ya maji kwa muda mrefu lakini sasa wanananchi wa mnarani na maeneo jirani  watanyamaza kilio cha shida hiyo.

Baadhi ya wananchi na wakaazi wa maeneo hayo wameelezea kufarijika kwa hatua hiyo kwani walikuwa katika wakati mgumu kwa muda mrefu

 

 

DK. ALI MOHAMED SHEIN AMETEMBELEA KIWANDA CHA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametembelea kiwanda cha Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Ras Al Khaimah“RAK GAS”iliyopo nje kidogo ya mji wa Ras Al Khaimah na kujionea shughuli za kiwanda hicho.

Katika kiwanda hicho ambacho kimekuwa kikifanya shughuli mbali mbali za kupokea gesi kutoka katika maeneo maalum ya uchimbaji, kuisambazasambamba na kuihifadhi kwa lengo la kuweza kuitumia.

Akiwa na ujumbe wake, Dk. Shein alipata maelezo kutoka kwa viongozi wa Kampuni hiyo ya KimataifayaUtafitinaUchimbajiwaMafutanaGesiAsiliayaRas Al Khaimah“RAG GAS”akiwemo Meneja Mkuu Peter Deibel, Msaidizi Meneja Mwendeshaji  Jody Labbie na Mwangalizi Mkuu wa Uzalishaji Deepu Thomas ambaye alitoa ufafanuzi juu ya uzalishaji pamoja na usambazaji wa gesi asilia kiwandani hapo.

Rais Dk. Shein alieleza kuvutiwa na shughuli mbali mbali zinazofanywa na kiwanda hicho katika eneo hilo lililopo nje kidogo ya mji wa Ras Al Khaimah ambalo ni muhimu katika shughuli za gesi asilia ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Ras Al Khaimah.

Alipongezahatua kubwa za maendeleo pamoja na mchango mkubwa wa mradi huo wa gesi kwa uchumi na maendeleo ya Ras Al Khaimah unatokana na mikakati madhubuti iliyowekwa katika kuhakikisha juhudi hizo zinachangia na kuendeleza soko la ajira, ukuaji wa uchumi na maendeleo ya viwanda katika nchi hiyo.

Viongozi hao wa kiwanda hicho cha Kampuni ya “RAG GAS” walimueleza Rais Dk. Shein shughuli mbali mbali zinazofanywa katika eneo hilo la kiwanda cha gesi na kutoa maelezoyanayohusiana na usafirishwaji kutoka maeneo inayozalishwa gesi hiyo hadi kiwandani hapo.

Aidha, walimueleza Rais Dk. Shein hatua na njia zinazotumika kusafirisha gesi hiyo asilia kutoka kiwandani hapo hadi katika maeneo inayotumika ambapo kwa maelezo ya viongozi hao wakuu Kampuni ya “RAG GAS”, gesi hiyo imekuwa na mchango mkubwa wa uchumi wa Ras Al Khaimah.

Viongozi hao walimueleza Rais Dk. Shein pamoja na ujumbe wake kuwa gesi hiyo imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa katika matumizi ya ndani ya nchi na nje ya Ras Al Khaimahsambamba na kuhangia katika kuimarisha viwanda vikiwemo viwanda vya saruji pamoja na viwanda vya vifaa vya ujenzi.

Kwa maelezo ya viongozi wa Kampuni hiyo ya “RAG GAS”, Ras Al Khaimah imekuwa ikichangia sana katika sekta ya ujenzi kwa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kutokana na rasilimali mbali mbali zinazozalishwa nchini humo.

Walieleza kuwa rasilimali hizo zimeweza kuendeleza viwanda na kukuza uchumi mchanganyiko, kukuza soko la ajira pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa mbali mbali zinazozalishwa nchini humo ambazo zina ubora mkubwa na zimekuwa maarufu sana duniani.

Mapema katika ukumbi wa Hoteli ya Waldorf Astoria mjini Ras Al Khaimah,  Rais Dk. Shein akiwa na viongozi wa ujumbe aliofuatana nao walikutana na viongozi wa ngazi za juu wa Kampuni ya “RAS GAS” na kumpa taarifa juu ya hatua zilizofikiwa katika utafiti wa mafuta na gesi asilia unaofanywa Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wakiongozwa na AfisaMtendajiMkuuwaKampunihiyoya“RAG GAS”NishantDighepamoja na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walizungumza juu ya hatua za kuendeleza zaidi ushirikiano katika utafiti, uendelezaji na uchimbaji wa nishati ya mafuta na gesi asilia Zanzibar.

Nao viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wao waliahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa lengo la kufikia mipango na mikakati iliyowekwa yenye tija kutokana  pande mbili hizo.

error: Content is protected !!