Daily Archives: April 15, 2019

WANAKIJIJI WA SHEHIA YA KIBUTENI WATOA PONGEZI KWA RAIS WA ZANZIBAR

Wanakijiji wa shehia ya kibuteni jimbo la makunduchi wametoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya ccm.

Wakizungumza na mwakilishi wa jimbo la makunduchi ambae pia ni waziri wa nchi ofisi ya Rais utumishi wa umma na utawala bora  Mhe Haroun Ali Suleiman wametaka salamu zao zimfikie Dk. Shein pamoja na wizara ya elimu na mafunzo ya amali kwa kufufua ujenzi wa skuli ya kibuteni uliokuwa umesita kwa zaidi ya miaka mitano.

Akizungumza na baadhi wajumbe washehia ya kubeteni mara baada ya kuangalia mradi wa barabara ya kifusi kuingia mji mpya na ujenzi wa kiwanja cha michezo  mwalimu Haruon amesema ujenzi wa barabara utasaidia kufanikisha azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kuwawekea miundo mbinu bora wananchi wake

Akizungumzia ujeni wa kiwanja cha michezo amesema huo ni mpango wa kuunga mkono juhudi za Rais wa Zanzibar Dk Shein katika ujenzi wa viwanja kila wilaya

Kwa upande wa wanakijiji hao hawakusita kutoa neno katika ujenza wa barabara na kiwanja.

MOTO MKUBWA WAZUKA NA KUTEKETEZA MALI NA VITU MBALI MBALI

Moto mkubwa uliozuka usiku wa jana umeteketeza mali na vitu mbali mbali katika nyumba ya ghorofa mbili katika mtaa wa malindi mjini Unguja.

Majira ya saa nne na nusu za usiku wa jumamosi, nyumba hii inayomilikiwa na Bw. Fahmi Ali Seif iliyopo eneo la nyuma ya msikiti wa ijumaa malindi, imeteketea kwa moto

WAKAAZI WA SHEHIYA ZA MSUKA WAMETAKIWA KUTHAMINI JUHUDI ZA SERIKALI

Wakaazi wa shehiya za msuka wametakiwa kuthamini juhudi za serikali na mashirika ya kujitolea katika kuzitumia fursa za maendeleo ili kuwanufaisha wananchi na kuwapunguzia ukali wa maisha .

Hayo yamesemwa na afisa elimu wilaya ya micheweni Bi Tarehe Khamis Hamad huko msuka katika mkutano wa mpango shirikishi wa kuainisha changamoto na kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya watu wa huko iliyondaliwa na shirika la milele Zanzibar foundation

Afisa huyo amesema ni jambo la kufurahisha kuona wananchi wanaisaidia serikali kwa kushiriki kwenye mipango ya maendeleo yao

Katika mkutano huo mratibu wa miradi ya afya wa Zanzibar milele foundation Shemsa Nassor Mselem amesema kupitia mpango huo wananchi wa msuka watafaidika na usaidizi wa miradi watakayoibua wao wenyewe kupitia shirika hilo

Nao baadhi ya wananchi hao wamesema wamefurahishwa kwa kufikiwa na mpango huo ambao wataweza kujiamulia kile ambacho wamekipa kipaumbele katika changamoto zao