Daily Archives: April 9, 2019

HATUA YA ROBO FAINALI LIGI YA VILABU BINGWA BARANI ULAYA

Hatua ya robo fainali ligi ya vilabu bingwa barani ulaya inatarajiwa kuanza kesho mzunguko wa kwanza kwa kuchezwa michezo miwili kwenye viwanja 2 tofauti majira ya saa 4:00 za usiku.

Majogoo wa anfield timu ya liverpool watakuwa na kazi kucheza na timu ya fc porto ya ureno mchezo utakaochezwa huko uengereza kwenye uwanja wa anfild.

Mchezo mwengine kesho muda huo huo utawakutanisha miamba miwili ya england kati ya totenhmah hotspurs dhidi ya manchester city.

Mashindano hayo yataendelea tena jumatano ambapo kutakuwa na shughuli pevu manchester united kucheza na barcelona mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani.

Nao ajax ya uholanzi itawaalika vibibi vizee vya turine italy timu ya juventus ambapo michezo hiyo pia itachezwa majira ya saa 4:00 za usiku.

YANGA SC IMEZINDUKA BAADA YA USHINDI WA MABAO 2-0 DHIDI YA AFRICAN LYON

Yanga sc imezinduka baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya african lyon jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Ushindi huo wa kwanza katika Ligi Kuu ndani ya mechi tatu, wakitoka kufungwa 1-0 na Lipuli na kutoa sare ya 1-1 na Ndanda FC, zote ugenini unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 71 baada ya kucheza mechi 30.

Maana yake, Yanga SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 11 zaidi ya Azam FC waliocheza mechi 30 pia wanaofuatia kwenye nafasi ya pili, mbele ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 57 za mechi 22 tu.

Mabao yote ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Heritier Ebenezer Makambo ambaye yupo katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka FC Saint Eloi Lupopo ya kwao.

Bao la kwanza alifunga dakika ya tano ya mchezo akimalizia pasi ndefu ya beki wa kati, Kelvin Patrick Yondan na la pili dakika ya 31 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu wa kiungo Haruna Moshi ‘Boban’.
Kipindi cha pili Yanga SC iliendelea kupeleka mashambulizi langoni mwa African Lyon, lakini ikaishia kukosa mabao ya wazi mfululizo.

MATOKEO MABAYA YA WANAFUNZI YAMECHANGIWA NA WALIMU WALIOSHINDWA KUWAJIBIKA

Wazazi wa wanafunzi wanaosoma skuli ya msingi na sekondari ng’ambwa, wamesema matokeo mabaya ya wanafunzi kwa mwaka 2018, yamechangiwa na walimu ambao wameshindwa kuwajibika pamoja na kuwatolea maneno ya jeuri wazazi wanapofuatilia maendeleo ya watoto wao.

Matokeo mabaya ya mitihani ya taifa katika skuli hiyo yamewafanya wazazi kukutana kujadili mbinu na mikakati ya kuongeza idadi ya ufaulu ambapo mzee haji hamad kombo na robart miguwa pamoja na katibu tawala wilaya ya chake chake omar khamis juma wamesema ujeuri wa walimu pamoja na kukosa uzalendo ndio sababu ya matokeo hayo.

afisa elimu na mafunzo ya amali wilaya ya chake chake , abadalla omar muya amewataka walimu kuandika barua kujieleza na kuzifikisha ofisini kwake si zaidi ya siku ya jumatano, huku mwalimu asma ali hafidh akielezea kutoridhishwa na matumizi ya simu kwa wanafunzi.

Mkuu wa wilaya ya chake chake rashid hadid rashid akizungumza kwenye mkutano huo amewataka wazazi kumpa ushirikiano ili kufanikisha kudhibiti utoro wa wanafunzi.

Mkutano ni moja ya mkikati ya serikali ya wilaya ya chake chake kuhakikisha inadhibiti utoro wa wanafunzi na kuongeza ufaulu wa wanafunzi

(SIDO) KUVIWEZESHA VIWANDA VIDOGO

Waziri wa viwanda na biashara joseph kakunda amelitaka shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini (sido)  kuviwezesha viwanda vidogo, kwani  hakuna nchi iliyoweza kufikia maendeleo ya viwanda bila kuanzisha viwanda hivyo.

Kakunda ametoa kauli hiyo jijini dar es salaam wakati akizundua bodi mpya ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo (sido) ambapo amesema hakuna sekta yeyote inaweza kukuua bila kuwepo kwa viwanda.

Nae mwenyekiti wa bodi ya sido prof. Elifax tozo bisanda amesema bodi inatarajia kuangalia upya mpango mkakati wa sido ili uweze kuendana na wakati.

Bodi ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo (sido) inaundwa na wajumbe sita na mwekitiki wake prof elifax tozo bisanda.