Serikali ya mapinduzi Zanzibar, itaendelea kulinda viwanda vyake ili kuhakikisha sera ya viwanda inatekelezwa kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa jumla.
Amesema mataifa yaliyoendelea yamefikia hatua hiyo kutokanan na kuwa na viwanda na kwamba Zanzibar itaimarisha viwanda mbali mbali vikiwemo vya kusindika matunda zikiwemo tungule.
Waziri wa wizara ya biashara na viwanda, Balozi Amina Salum Ali, ameyaema hayo wakati akizungumza na ushirika wa mtule amcos limited katika kijiji cha Paje ulionzisha kiwanda cha kutengeneza tomato paket .
Amesema serikali itaendelea kuhakikisha inasaidia nguvu wananchi wake wakiwemo wakulima ili kuona wanapata kipato kupitia viwanda vya ndani.
Akisoma risala ya wanaushirika wa mtule amcos limited katibu wa ushirika huo, Ali Fadhil Ali, amesema ushirika wao unakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo umalizaji wa kiwanda na upatikanaji wa vibali kutoka mamlaka husika ikiwemo ZBS na TBS.
Ushirika huo una wanachama 139 wakiwemo wanawake 52 na wanaumme 87 ambapo kila mmoja anamiliki shamba lake la zao la tungule.