Daily Archives: April 3, 2019

WAMILKI WA HOSPITALI BINAFSI WATAKIWA KUENDELEZA MASHIRIKIANO

Wamilki wa Hospitali binafsi wametakiwa kuendeleza mashirikiano na uongozi wa bodi ya ushauri ya Hospitali binafsi ili kufanikisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza na wamiliki na wafanyakazi wa Hospitali hizo mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Hospitali binafsi Dr Jamala Adam amesema Hospitali binafsi zimekuwa na mchango mkubwa katika kuisaidi Serekali pamoja na wananchi wake.

Dk Jamala amefahamisha kuwa katika kufanikisha utenndaji wao ni vyema  wakafuata taratibu na sheria zilizoekwa.

Baadhi ya wajumbe walioshiriki mkutano huo wameuomba uongozi wa bodi kuandaa utaratibu mzuri wa ukaguzi kwa vile kumekuwa na malalamiko mengi kwa wananchi juu ya huduma hafifu kwa baadhi ya hospitali.

Kwa upande wake Nd Khamis Haji Makame msaidizi mrajis wa bodi ya ushauri ya Hospitali binafsi amesema mkutano huo unalengo la kutoa utekelezaji wa kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja .

Jumla ya hospitali 2 moja Unguja na moja Pemba zimekabidhiwa vyeti kwa utoaji wa huduma bora pamoja na kuwa na ubora wa hali ya juu.

(TMA) IMESAINI MKATABA WA UFUNGAJI WA RADA MBILI ZA HALI YA HEWA NA (ECC)

Mamlaka ya hali ya hewa tanzania (TMA) imesaini mkataba na kampuni ya enterprise electronics corporation (ECC) wa ufungaji wa rada mbili za hali ya hewa.

Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania DKT Agnes Kijazi na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya enterprise electronics corporation (ECC) edwin kasanga.

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo naibu Waziri wa wizara ya ujezi uchukuzi na mawasiliano atashasta ndindiye amesema rada hizo zitafungwa katika mikoa ya mbeya na kigoma na ujezi wake utakamilika ndani ya miezi kumi na nne.

Aidha naibu Waziri ndindiye amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha usahii wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa unafikia asilimia 99 ambapo kwa sasa nia asilimia 88.

Nae mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya enterprise electronics corporation (ECC) Edwin Kasanga ambao niwatekelezaji wa mradi huo amesema kampuni hiyo itatekeleza majukumu kwa mujibu wa mkataba.

Kufungungwa kwa rada hizo kutaipelekea Tanzania kuwa taasisi bora kwa ungalizi wa hali ya hewa kwa njia ya rada katika ukanda wa afrika mashariki na kati.

JAMII IMETAKIWA KUJITOLEA KWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA HARAKATI ZA KUKABILIANA MAAFA

 Jamii imetakiwa kujitolea kwa kutoa ushirikiano  katika harakati  za kukabiliana maafa pamoja na uokozi katika mazingira  ya baharini ili kuwa salama na kuepusha  vifo vya mara kwa vinavyotokea.

Hauli hiyo imetolewa na  mkuua kitengo cha upersheni kukabiliana na maafa wakati wa semina ya kujadili masula mbali mbali juu ya kujifunza kuogelea na uokozi.

Amesema vifo vingi vimekuwa vikitokea sehemu za baharini na maziwa hivyo kupitia mafunzohayowanaweza kujikinga na matukio ya maji.

Mkurungenzi wa Panje Bi  Mwanaidi Abdallah amesema   wameweza kutoa mafunzo mbali mbali kwa wanafunzi elfumbili  miasita na thalathini na tano kwa Unguja na Pemba na kuwaomba jamii wawena utamaduni kwa kujifunza kuogelea ili kunusuru vifo  na majanga yanayoweza kutokea.

Baadhi ya washiriki wa lioshiriki katika semina hiyo wamesema kuwe kunawekwa mikakati maalumu kwa vijana  nawazee kujifundisha kuogelea kwani wanawake wengi wamekuwa wakipoteza maisha yao wakati wakienda kulima mwani.