WAKULIMA WA MWANI WA KIJIJI CHA PAJE WAPATA KHOFU JUU YA KILIMO CHAO

Wakulima wa mwani wa kijiji cha paje wameuomba uongozi wa wizara ya kilimo kupitia idara ya maendeleo ya uvuvi kuangalia harakati za watalii za michezo ya baharini katika fukwe za paje kwani zimeanza kuwajengea hofu juu ya kilimo chao cha mwani.

Wakulima hao wameiambia ZBC kuwa watalii wanafanya   michezo ya maputo smoklin karibu na maeneo ya fukwe wakati ambapo kilimo cha mwani kikiwa kinaendelea.

Wamesema kuwa ingawa utalii una faida sana katika taifa  lakini ni vyema taasisi husika zikakaa pamoja kuwapangia maeneo maalum ambayo wao watafanya michezo yao hiyo  na harakati za kilimo cha mwani zikiendelea.

Akilitolea ufafanuzi suala hilo mkurugenzi idara ya maendeleo ya uvuvi Nd Mussa Aboud Jumbe amesema watakaa pamoja na mamlaka ya uwekezaji ili kutafuta muafaka wa tatizo hilo bila ya kutokea athari yoyote.

No Comments Yet.

Leave a comment