VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUANZISHA VIPINDI VINAVYO HAMASISHA KUSOMA

Waziri wa elimu mafunzo ya amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma amewataka wamiliki wa vyombo  vya habari  kuanzisha vipindi  vinavyo hamasisha kusoma na sio kutoa burudani pekee.

akizungumza katika uzinduzi wa kapmeni ya tukutane skuli   amesema wasikilizaji na watazamaji wakubwa ni wanafunzi hivyo ni vyema kwa wamiliki wa vyombo hivyo kutoa vipindi vya elimu ili ufaulu wa wanafunzi uzidi kuongezeka.

mkuu wa mkoa wa mji maghribi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud amekipongeza kituo cha *zenji media group* kwa kuanzisha kipindi cha *tukutane skuli* ambacho kitawasaidia wanafunzi kujua wajibu wao katika kutafuta elimu.

nae meneja wa mradi wa *tukutane  skuli* Ndg.Yussuf Mohamed amesema iegno la kuanzisha kipindi hicho ni  kuwashajiisha vijana  hasa wanafunzi kuweza kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao.

 

Comments are closed.