UFAULU WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2018 UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 1.9

Naibu Katibu Mkuu Taaluma Wizara Elimu na Mafunzo ya Mali Zanzibar Ndg. Madina Mjaka Mwinyi amesema ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2018 umeongezeka kwa asilimia 1.9 ukilinganisha na mwaka 2017.

Akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2018 kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa wa wizara hiyo mazizini amesema takwimu za matokeo zinaonesha kuwa ufaulu umepanda kwa baadhi ya masomo kwa asilimia 0.83 hadi 8.76 ikilinganishwa na mwaka 2017.

Aidha amesema pamoja na kuongezeka kwa asilimia ya ufaulu, takwimu kwa upande wa masomo ya commerce, hesabati, physics, na book- kiping upo chini ya asilimia hamsini 50%.

Amezitja  skuli 10 zilizofanya vizuri kwa upande wa zanzibar miongoni mwao kuwa ni lumumba, fidel castro, laurent, tumekuja na sos. Na zile zilizo fanya vibaya ni p/ mchangani, ukutini, kijini, ng’ambwa na hamamni.

Jumla ya watahaniwa 16,654  sawa na asilimia 97.4 walifanya mtihani  na 444 sawa na asilimia 2.6 hawakufanya mtihani mwaka 2018 kwa sababu tofauti.

Comments are closed.