SEKTA ZILIZOGATULIWA KUSINI PEMBA ZAKABILIWA NA MATATIZO YA WAFANYAKAZI NA VITENDEA KAZI

Wafanyakazi wa sekta zilizogatuliwa Mkoa wa kusini Pemba wamesema wanakabiliwa na matatizo ya wafanyakazi na vitendea kazi hivyo wameiomba serikali kuwatatulia matatizo hayo ili kufanikisha majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti mbele ya Waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz mheshimiwa Haji Omar Kheir kwenye mikutano ya kusikiliza matatizo yanayozikabili sekta zilizogatuliwa  kisiwani Pemba

Wamesema katika kuona maendeleo yanazidi kuimarika ni vyema kwa serikali kubuni nafasi zaidi za ajira na kuzitafutia ufumbuzi  changamoto ndogo ndogo zilizopo.

Katika ziara hiyo waziri afisi ya rais tawala za Mikoa serikali za mitaa na idara maalum za SMZ mheshimiwa Haji Omar Kheir amesema kwa kushirikiana na viongozi wengine watakaa kuyafanyia kazi matatizo yaliopo ili kuona sekta hizo zinasonga mbele kama ulivyo mpango wa serikali wa kuwaletea wananchi wake huduma karibu nao .

Amesema katika  kuimarisha dhana ya ugatuzi  serikali imepanga katika  bajeti ya  2019-2020 kujenga madarasa 600 unguja na Pemba ili kukidhi haja ya ukosefu wa vyuma vya kusomea

Mapema Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdalla amewataka wafanyakazi hao kuzidi kujituma huku serikali ikiendelea kuzitafutia ufumbuzi wa kina changamoto zao.

Comments are closed.