MRADI WA JUMUISHO KUWANUFAISHA WATU WENYEULEMAVU

Mkurugenzi Idara ya Watu wenye ulemavu Bi Abieda Rashid amesema Serikali  kupitia idara yawatu wenye ulemavu inaunga mkono  na kushirikiana pamoja   katika kufanikisha  mradi wa jumuisho wa kijamii maendeleo  kwa watu wenye ulemavu ili kuweza kupata mabadiliko kwa watuwenye ulemavu kwa kushirikishwa kwa kuweza kupata huduma bora za kijamii kwa watu wenye ulemavu.

Bi Abieda ameyasema hayo katika ukumbi wa watu wenye ulemavu kikwajuni mini unguja wakai wa ufunguzi   kwenye mkutano wa tasisisi  za kiraia na  jumuiya ya watu wenye ulemavu kutoka nchi ya nowroy.

Amesema mkutano huo utajadili masuala mbali mbali ya kijamii inayowahusu Watu wenye ulemavu kwa kuweza kupata haki zao za msingi  na kuuchumi kwa kushirikishwa katika mambo mbali mbali ya maendeleo kwa kusimamia huduma za watu wenye ulemavu.

Mkurugenzi wa mradi wa madrasa Early Chidhood Program Ndugu Khamis Abdalah Saidi amesema mradi huo utasaidi kutoa malengo muhimu  za haki sawa kwa  watuwenye ulmavu ikiwemo elimu afya pamoja na ajira   na kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili watu wenye ulemavu.

kwa upande wa mlemavu asioona kutoka malawi Ndugu  Munyaras Mulalo amesema ameweza kufaidika  na misaada inayotolewa na  shirika la kimataifa  la marekani linoshugulikia wutu wenye ulemavu kwa kuanzisha program mbali mbali  na kuweza kusaidia jumuiya nyengine.

 

Comments are closed.