MPANGO MAALUM WA KUWEKA MIUNDOMBINU BORA YA USALAMA KWENYE VITUO VYA MAFUTA

Wamiliki wa vituo vya mafuta kisiwani pemba wametakiwa kuwa na mpango maalum wa kuweka miundombinu  bora ya usalama kwenye vituo hivyo ikiwemo kuwapa mafunzo wafanyakazi wao na kuweka vifaa vya huduma ya kwanza ili waweze kujiokoa panapotokezea matatizo.

Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na mkuu wa operation ya kukabiliana na maafa zanzibar Shaaban Hassan Ramadhan katika ziara ya ukaguzi wa bohari na vituo vya mafuta kisiwani humo

Amesema katika ukaguzi huo wamegundua mapungufu mengi ya kiusalama huku akitoa agizo la miezi mitatu kwa wamiliki kuyafanyia kazi mapungu hayo kabla ya kutokea maafa yasiyotarajiwa

Katika ziara hiyo mkuu wa operation ya uokozi kutoka kikosi cha zimamoto ali abdi hashim amesema baadhi ya vituo havina dawa mitungi ya kisasa ya kuzimia moto wala matangi ya maji hivyo kuwa vigumu kwao kuweza kujisaidia kunapotokea tatizo

Nao baadhi ya wasimamizi wa vituo hivyo vya mafuta wamesema watayafanyia kazi mapungufu madogo madogo yaliopo na yale makubwa watawasiliana na wamiliki wao kwa ajili ya kuyachukulia hatua

No Comments Yet.

Leave a comment