MHE SALAMA ABOUD TALIB AMEITAKA KAMATI ENDESHI YA MAMLAKA YA MJI MKONGWE KUFANYAKAZI KWA PAMOJA

Waziri wa ardhi nyumba maji na nishati Mhe Salama Aboud Talib ameitaka  kamati endeshi ya mamlaka ya mji mkongwe kufanyakazi kwa pamoja ili kuhakikisha inazipatia ufumbuzi kasoro zitakazoisababisha zanzbar kungia katika orodha za nchi zinazotaka kuondolewa katika urithi wa kimataifa.

Waziri Salama Aboud ameeleza hayo katika mkutano wa uzinduzi wa kamati endeshi ya mamlaka ya mji mkongwe yenye wajumbe 14 kutoka Zanzibar na Tanzania bara kutoka katika tasisi mbali mbali ikiwemo uwekezaji,bandari ,makumbusho na mambo ya kale,mazingira,utalii, manispaa wakfu na urithi wa dunia.

Amesema anaamini kuwa kamati hiyo yenye wataalamu ambao wanauzoefu itasaidia kuondoa vikwazo hivyo  kwa muda mfupi na kuuwezesha mji mkongwe kubaki katika historia yake ya asili na kuundelea kuwa urithi wa kimataifa.

Akizungumza katika mkutano huo donatius kamamba kutoka kituo cha urthi wa dunia tanzania amesema kamati ya urithi wa dunia imeona umuhimu wa kuishauri serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuunda kamati itakayosaidia kuondoa kasoro  hizo.

Mkuu wa mamlaka ya mji mkongwe Zanzibar Issa Sariboko makarani amesema kamati hiyo itahakikisha mpango mkuu mpya wa uhifadhi utajumuisha mipango mengine ya kitaifa na kanda ya afrika katika kuhifadhi thamani ya kipekee ya mji mkongwe.

Comments are closed.