MASHUA YA PLASTIKI IMEIWEKA ZANZIBAR KATIKA RAMANI YA DUNIA

 

Ujio wa Mashua ya Mazingira Iliyotengenezwa kutokana na Malighafi ya Plastiki kutoka Nchini Kenya Chini ya Ushauri wa Taasisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa unaiweka Zanzibar katika Ramani ya Dunia kwenye Mapambano yake Dhidi ya Uchafuzi wa Mazingira.

Mashua hiyo ambayo tayari imeshaondoka jana kutoka mombasa nchini kenya inaingia Wete Kisiwani Pemba, kupitia Mkoani Pemba, Nungwi Mkoa Kaskazini Unguja na kutarajiwa kuingia  Forodhani Mjini Zanzibar mnamo tarehe 6 mwezi huu.

Kikao cha Washirika wanaosimamia na kushughulikia masuala ya Mazingira kutoka Taasisi za Umma, Binafsi pamoja na zile za Kimataifa  walikutana kujadili ujio wa Mashua hiyo chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi kilichokutana Vuga Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja aliwaelezea Wajumbe wa Kikao hicho kwamba lengo la Mashua hiyo ni kuihamasisha Jamii juu ya kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira yanayoleta Mabadiliko ya Tabia Nchi Duniani.

Nd. Mjaja alisema Tarehe 7 Febuari siku Moja baada ya kuwasili Mashua hiyo kutakuwa na uzinduzi wa usafi wa Mazingira katika Ufukwe wa Forodhani utakaoshirikisha Taasisi tofauti zinazojishughulisha na masuala ya Mazingira Zanzibar.

Naye kwa upande wake Ofisa wa Uratibu katika masuala ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bibi Clara Makenya alisema usafishaji wa Mazingira katika Pwani ya Forodhani itaongozwa na Muungano wa Taasisi za Kimazingira ya Les Do It Company Zanzibar.

Comments are closed.