MAJAJI NA MAHAKIMU WANATAKIWA KUENDESHA KESI KWA HARAKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe, Haroun Ali Suleiman amewataka Majaji na Mahakimu Kuendesha Kesi kwa Haraka ili Wananchi WawezeKupata haki zao katika kipindi  kifupi.

Amesema kufanya hivyo Itaonyesha Uwajibikaji wa Haraka katika Utekelezaji wao wa usimamizi waSheria katika kuwapatia haki kwa wananchi na hivyo wananchi kujenga imani na tasisi hiyo

Akifungua Maonesho yaMaadhimisho ya Sku ya Sheria huko Gombani Chake Chake, Mhe Haroun amewahimiza Wananchi kuyatumia Maonesho Hayo kwa kujifunza na kufahamu Taratibu Sahihi za kujua haki zao na jinsi ya kuzipata.

Amesema Fursa hiyo Iitumiwe na Majaji na Mahakimu  kuwashauri wananchi katika Kutatua Matatizo yao kwa kushirikia na sekta  ya Sheria ili kujuwa Njia za kuyatatua bila ya kuwepo kwa migogoro.

Aidha Mhe, Haroun Amekemea Vitendo vya Unyanyasaji Vinavyojitokeza kila siku hasa kwa Watoto na kuwahimiza Mahakimu kuangalia Sheria  na kuzitumia kwa Kuviangamiza Vitendo hivyo.

Akizungumzia Maonesho hayo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu Amesema Maonesho hayo kufanyika Pemba ni Utekelezaji wa Agizo la Rais Dk. Shein kuitaka mahkama kuyafanya kisiwani humo ili wananchi wanufaike baada ya kufanyika kisiwani unguja takribani mara mbili.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdalla kwa Niaba ya Wananchi amesema maonesho kufanyika Gombani ni moja ya Mafanikio na Mashirikiano kati ya Tasisi za Umma na Jamii.

 

Comments are closed.