HATUA ZITACHUKULIA KWA WAMILIKI WA HEKA AMBAO WATABAINIKA NA UUZAJI WA VIWANJA

Mkuu wa wilaya ya kaskazini" B" Ndugu Rajab Ali Rajab amesema Serikali ya wilaya  yake itawachukulia  hatua  za kisheria wamiliki wa heka ambao watabainika  kuhusika na uuzaji  wa  viwanja  jambo ambalo ni kinyume na matumizi ya heka hizo.

Akizungumza na wakaazi wa kinyasini kisongoni  mara baada ya kutembelea heka yenye mgogoro kati ya familia ya Bi Mtumwa Ali  aliyemruhusu kujenga nyumba ya muda Bi Hadiya Ambar Riyami ambayo kwa sasa familia yake inakikuka masharti waliyopewa kwa kuendelea kujenga nyumba nyengine  ambapo ni kinyume na utaratibu wa matumizi ya heka

Amesema heka ni mali ya Serikali ambazo zimetolewa kwa Wananchi kwa ajili ya kuziendeleza kwa shughuli za kilimo na si kwa ajili ya makaazi kama baadhi ya watu wanavyozitumia.

Akizungumza kwa niaba ya familia ya Bi Mtumwa Ali mwanafamilia Bi fatma Khamis Ame amesema wanashangazwa na  kitendo  cha watoto wa Bi Hadia Ambar  kuendelea na ujenzi wa nyumba za kudumu  katika   heka hiyo  ambayo awali alipewa  Bibi  yao kujenga nyumba kwa muda.

Bibi Hadiya Ambar amesema sehemu hiyo amepewa akae na mwenye eka na kuhusu ujenzi wa nyumba zinazojengwa na watoto wake amesema nao pia wamepewa ruhusa ya kujenga na mmiliki wa heka hiyo.

Comments are closed.