HATUA ZA KISHERIA KUCHUKULIWA KWA MTU YEYOTE ATAKAYE KUTWA AMEMUAJIRI MTOTO

Mkuu wa wilaya ya micheweni Pemba Salama Mbaruk Khatib amepiga marufuku vitendo vya kuwapa ajira watoto vinavyofanywa na baadhi ya wavuvi katika bandari za wilaya hiyo hali inayosababisha watoto hao kukosa haki zao za msingi ikiwemo elimu.

Mkuu huyo wa wilaya, ameitoa kauli hiyo katika ziara ya kutembelea bandari ya shumba mjini na kuzungumza na wazee na wanunuzi wa samaki katika bandari hiyo baada ya kubainika kuwepo kwa watoto wanaofanyishwa kazi kinyume na sheria.

Mkuu huyo wa wilaya ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mtu yeyote atakaye kutwa amemuajiri mtoto.

Hadia Juma Kombo mkaazi wa shehia ya shumba ya mjini amesema analazimika kuwachukua watoto ili wamsaidie baadhi ya kazi ikiwemo uvunaji wa mwani kutokana na mume wake kushindwa kumsaidia kuwatunza watoto hao.

 

Comments are closed.