Category Archives: Michezo na Burudani

SHILINGI MILIONI 10 ZAGAIWA KWA TIMU YA TAIFA YA MPIRA WA MIGUU YA WATU WENYE ULEMAVU

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa shilingi milioni 10 kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya  watu wenye ulemavu inayojiandaa kushiriki mashindano ya afrika   kuanza tarehe 01 mwezi ujao, mwaka huu nchini angola.

Katibu wa rais, wa Tanzania  ngusa samike amekabidhi fedha hizo kwa viongozi na wachezaji wa timu hiyo katika hafla iliyofanyika studio za shirika la utangazaji tbc.

Wamesema timu hiyo yenye wachezaji 13, walimu 5 na viongozi 2 itaondoka tarehe 28 mwezi huu,  kuelekea nchini angola ambako inakwenda kushiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza huku wakiahidi kufanya vizuri.

WAWAKILISHI WA ZANZIBAR KWENYE MASHINDANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA

Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Malindi wameanza vibaya nyumbani baada ya kukubali kufungwa mabao 4-1 dhidi ya Almasry ya Misri mchezo uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan.

Mabao ya Almasry yamefungwa na Mahmoud Wadi dakika ya 27, 39, Hassan Ibrahim dakika ya 32 na Saidou Simpore dakika ya 52 huku bao pekee la Malindi likifungwa na Ibrahim Ali (Imu Mkoko) dakika ya 42.

Mchezo wa marudiano utachezwa Septemba 29, 2019 huko Misri ambapo Malindi anatakiwa kushinda 4-0 ugenini ndipo asonge mbele.

 

CHAMA CHA SOKA MKOA WA KUSINI UNGUJA (SOURFA) IMETANGAZA MAJINA YA WAJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI

Chama cha soka mkoa wa kusini unguja (SOURFA) imetangaza majina ya wajumbe wa kamati ya uchaguzi watakaosimamia uchaguzi wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya kusini unguja (KUDFA) na wilaya ya kati (KADFA).

Akitangaza kamati hiyo makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa kusini unguja Abubakar Khatib Kisandu amemtaja khamis hamza khamis kuwa mwenyekiti, Mshimba Seif Mshimba (katibu) na wajumbe ni ramadhan mrisho na issa suleiman mzee.

Kisandu amesema kamati hiyo imepewa dhamana ya kusimamia chaguzi zote mbili ya kati na kusini ambapo wanatakiwa kufanya chaguzi hizo si zaidi ya septemba 30, 2019.

WAZEE, WALEZI PAMOJA NA WADAU WA MICHEZO WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA KUIBUA VIPAJI VYA VIJANA

Wazee, walezi pamoja na wadau wa michezo   wametakiwa kushirikiana kuibua vipaji vya vijana vilivyojificha katika michezo hasa maeneo ya vijini kwani  michezo imekuwa ikitoa fursa nzuri ya ajira  na kujikwamua kiuchumi.

Wito huyo umetolewa na mjumbe wa NEC Taifa nd Ramadhani Shaibu Juma  wakati alipokuwa akikabidhi vifa vya michezo na kusherekea ushindi kwa  timu ya fast fast ya  kangangani iliyoibuka na ubingwa katika  kombe la kangangani cup.

Amesema michezo ni ajira endapo vijana hao wataendelezawa vizuri kwa  kutumia vipaji vyao wanaweza kujiri wenyewe kupitia michezo na kuendeleza utamaduni.

Mapema afisa kitengo cha uratibu chama chama pinduzi ccm pemba   mabaye pia ni mlezi wa timu hiyo zulefa abdall said ameipongeza timu ya fasta fast kwa haraka zao za kukimbilia ubingwa kama lilivyo  jina lao    kwa kupata ubingwa huo  kwani mbio za sakafuni hazikuishia ukingoni.

Nao wanachezo wa timu hiyo wamesema licha ya kuibuka na ubingwa huyo ila bado wanakabiliwa na changamoto  mbali mbali ikiwemo ya vifa vya  michezo.