Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

SMZ INAKUSUDIA KUTEKELEZA MPANGO WA KUKAMILISHA KITOVU CHA MJI

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kutekeleza mpango wa kukamilisha kitovu cha mji ambao utasaidia  kuimarisha mji na kuufanya kuwa kichocheo cha biashara na uwekezaji.

Mkurugenzi Idara ya mipango miji Dk Muhammad Juma ameeleza hayo wakati akiwasilisha mada katika Mkutano wa kuutambulisha mipango huo kwa Masheha wa shehia 13 za Wilaya ya Mjini.

Dk Juma amesema lengo la mradi huo ni kutekeleza azma ya Rais wa kwanza Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kwa kuuendeleza mji na kuwa kichocheo cha uwekezaji na biashara kama zilivyo nchi nyengine.

Mkuu wa wilaya ya mjini Bi Marina Joil Tomas amewataka masheha kuwaelimisha wanananchi juu ya azma hiyo ya serikali ya kuimarisha mji.

Masheha wameomba idara ya mipango mji na manispaa zifanye kazi sambamba ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kujitokeza katika mradi huo.

 

 

SMZ NA WASHIRIKI WA WARSHA

Ofisi ya uratibu shughuli za serikali ya mapinduzi Zanzibar (  SMZ) iliyopo jijini Dar es Salaam imewataka washiriki wa Warsha ya kuitambulisha Ofisi ya uratibu ,kutoa mawazo yatakayosaidia kuijenga ofisi hiyo ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na mratibu mkuu wa ofisi ya shughuli za SMZ  Issa Mlingoti wakati akifungua warsha hiyo amesema afisi  hiyo  ni kiiunganishi kati ya taasisis za Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mlingoti amesema kuwa taasisi yeyote yenye mafanikio lazima iwe na mashirikiano mazuri na taasisi za nje pamoja na kusikiliza mawazo na kuyafanyia kazi ili kuweza kuimarisha  au kujenga taasisi husika.

Wakiwasilisha mada, Afisa mratibu wa masuala ya habari utalii utamaduni michezo na afya , Aida  Osmond na Afisa Mratibu masuala ya Fedha na mipango Shumbana Ramadhan walisema kuwa misingi mkiuu ya utendaji ya ofisi ya uratibu SMZ iliyopo Dar es Salaam ,ni uadilifu uwazi na uwajibikaji katika upatikanaji wa huduma wakizungumzia  mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na  kutatua changamoto mbalimbali za kijamii ikiwemo migogoro ya wavuvi na ardhi.

kwa upande  mshiriki wa warsha hiyo afisa Mwitikio wa taasisi za Umma tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (tacaids) Dkt.Hafidh Ameir ameshauri kuunda kitengo cha afya kazini,ili kuweza kuwasaidia wafanyakazi.

Warsha hiyo ya siku moja imeandaliwa  na ofisi ya uratibu wa shughuli za serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ ) iliyopo Dar es Salaam imewashirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali zza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar zilizopo Dar es Salaam na Tanzania bara.

 

KUIMARISHWA ULINZI WA UHAKIKIKA KATIKA MAENEO YA MITAMBO YA REDIO ILIYOPO MASINGINI NA DOLE

Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale imependekeza kuimarishwa ulinzi  wa uhakikika  katika maeneo ya mitambo ya redio iliyopo masingini na dole  ili kuhakikisha  kuna uwa katika hali ya usalama zaidi   katika maeneo hayo.

Naibu Waziri wa  wizara hiyo Mh Bihindi Kombo Khamis  ameeleza hayo kufuatia ziara  ya kamati ya maendeleo ya wanawake habari na utalii ya baraza la wawakilishi baada ya kutembelea maeneo ya mitambo ya kurushia matangazo ya televisheni masingini na mitambo ya kurushia matangazo ya redio ya shirika la utangazaji zanzibar iliyopo dole.

Akizungumza katika kikao cha majumuisho Mh Bihindi amesema wizara ya habari utalii na mambo ya kale imekusudia  kutoa kipaumbele  kutekeleza  miradi yote  ya wizara katika kipindi cha bajeti  kinachotarajiwa kumalizika mwaka huu.

Akihitimisha ziara hiyo mwenyekti wa kamati ya maendeleo ya wanawake habari na na utalii ya baraza la wawakilishi Mh Mussa Fumu Mussa,  amesema kumekuwa na tatizo la waongozaji watalii ambao hawana vibali hali ambayo amesema ni tatizo kwa kamisheni ya utalii na kutaka kurekebishwa kasoro hizo.

WAFANYABIASHARA KUTUNZA MAZINGIRA NA KUIMARISHA USAFI

Wafanyabiashara wa vyakula katika manispaa ya mji wa zanzibar wametakiwa kutunza mazingira na kuimarisha usafi katika maeneo yao ya biashara ili kulinda afya za walaji.

Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa baraza la manispaa mjini nd. Said juma ahmada katika semina ya mafunzo kwa wafanyabiashara hao.

Amesema wafanyabiashara wa vyakula wanachukua jukumu kubwa la kulinda afya ya mlaji hivyo ni vyema kuzingatia taratibu za usafi katika uandaaji wa vyakula hivyo na kutengeneza miundombinu ya kufanyia biashara zao katika kipindi hichi cha mvua za masika.

Muezeshaji katika semina hiyo nd forogo mtande amewataka wafanyabiashara kuitumia kwa vitendo elimu waliyoipata   na kuifikisha kwa wenzao elimu hiyo bila ya kuipuuza ili kuepuka maradhi mbali mbali ikiwemo kipindupindu.

Wafanyabiashara walioshiriki katika semina hiyo wamelitaka baraza kuwapa elimu mara nyingi na kuwasimamia ili kuwa na uwelewa wa kutosha juu ya usafi na uhifadhi wa chakula.