Recent Posts by Fatma Muhamad

MAREKANI NA CHINA KUJIPA MATUMAINI YA KUWEZA KUTULIZA MVUTANO WAO

Marekani na China Wanaonyesha Kujipa Matumaini ya Kuweza Kutuliza Mvutano wao wa Kibiashara. Rais wa Marekani Donald Trump amesema baada ya Mazungumzo pamoja na Makamo wa Rais wa China Liu He,"makubaliano muhimu ya kibiashara yatafikiwa."Mjumbe wake katika mazungumzo ya biashara pamoja na China, Robert Lightizer amesema pia "maendeleo yameweza kupatikana" wakati wa mazungumzo yao. Rais Xi Jinping wa China ameandika katika risala yake anataraji pande hizo mbili zitaendelea kushirikiana katika hali ya kuheshimiana. Pindi makubaliano yakishindwa kufikiwa hadi Machi mosi inayokuja, rais Trump anapanga kuzitoza ushuru wa asilimia kati ya 10 na 25 bidhaa zote zitakazoingia Marekani kutoka China.

MAJAJI NA MAHAKIMU WANATAKIWA KUENDESHA KESI KWA HARAKA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe, Haroun Ali Suleiman amewataka Majaji na Mahakimu Kuendesha Kesi kwa Haraka ili Wananchi WawezeKupata haki zao katika kipindi  kifupi.

Amesema kufanya hivyo Itaonyesha Uwajibikaji wa Haraka katika Utekelezaji wao wa usimamizi waSheria katika kuwapatia haki kwa wananchi na hivyo wananchi kujenga imani na tasisi hiyo

Akifungua Maonesho yaMaadhimisho ya Sku ya Sheria huko Gombani Chake Chake, Mhe Haroun amewahimiza Wananchi kuyatumia Maonesho Hayo kwa kujifunza na kufahamu Taratibu Sahihi za kujua haki zao na jinsi ya kuzipata.

Amesema Fursa hiyo Iitumiwe na Majaji na Mahakimu  kuwashauri wananchi katika Kutatua Matatizo yao kwa kushirikia na sekta  ya Sheria ili kujuwa Njia za kuyatatua bila ya kuwepo kwa migogoro.

Aidha Mhe, Haroun Amekemea Vitendo vya Unyanyasaji Vinavyojitokeza kila siku hasa kwa Watoto na kuwahimiza Mahakimu kuangalia Sheria  na kuzitumia kwa Kuviangamiza Vitendo hivyo.

Akizungumzia Maonesho hayo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu Amesema Maonesho hayo kufanyika Pemba ni Utekelezaji wa Agizo la Rais Dk. Shein kuitaka mahkama kuyafanya kisiwani humo ili wananchi wanufaike baada ya kufanyika kisiwani unguja takribani mara mbili.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdalla kwa Niaba ya Wananchi amesema maonesho kufanyika Gombani ni moja ya Mafanikio na Mashirikiano kati ya Tasisi za Umma na Jamii.

 

MASHUA YA PLASTIKI IMEIWEKA ZANZIBAR KATIKA RAMANI YA DUNIA

 

Ujio wa Mashua ya Mazingira Iliyotengenezwa kutokana na Malighafi ya Plastiki kutoka Nchini Kenya Chini ya Ushauri wa Taasisi ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa unaiweka Zanzibar katika Ramani ya Dunia kwenye Mapambano yake Dhidi ya Uchafuzi wa Mazingira.

Mashua hiyo ambayo tayari imeshaondoka jana kutoka mombasa nchini kenya inaingia Wete Kisiwani Pemba, kupitia Mkoani Pemba, Nungwi Mkoa Kaskazini Unguja na kutarajiwa kuingia  Forodhani Mjini Zanzibar mnamo tarehe 6 mwezi huu.

Kikao cha Washirika wanaosimamia na kushughulikia masuala ya Mazingira kutoka Taasisi za Umma, Binafsi pamoja na zile za Kimataifa  walikutana kujadili ujio wa Mashua hiyo chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi kilichokutana Vuga Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja aliwaelezea Wajumbe wa Kikao hicho kwamba lengo la Mashua hiyo ni kuihamasisha Jamii juu ya kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira yanayoleta Mabadiliko ya Tabia Nchi Duniani.

Nd. Mjaja alisema Tarehe 7 Febuari siku Moja baada ya kuwasili Mashua hiyo kutakuwa na uzinduzi wa usafi wa Mazingira katika Ufukwe wa Forodhani utakaoshirikisha Taasisi tofauti zinazojishughulisha na masuala ya Mazingira Zanzibar.

Naye kwa upande wake Ofisa wa Uratibu katika masuala ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bibi Clara Makenya alisema usafishaji wa Mazingira katika Pwani ya Forodhani itaongozwa na Muungano wa Taasisi za Kimazingira ya Les Do It Company Zanzibar.

NAIBU WAZIRI AKABIDHI VIFAA KWA KIKUNDI CHA TAIFA CHA TAARAB

Naibu Waziri wa Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo Lulu Msham Abdalla amesema Wizara yake itahakikisha kikundi cha Taifa cha Taarab kinafanya kazi zake vizuri ili kuendelea kukuza sanaa ya Muziki wa Tarab Visiwani hapa.

Amesema asilimia kubwa ya wananchi wa Zanzibar katika mkiaka ya zamani walikuwa ni wapenzi wa muziki wa Tarab Asilia kama ilivyokuwa wakazi wa Tanga na Mombasa na kwamba Serikali inataka hali hiyo iendelee kuwa hivyo

Naibu waziri huyo ameyasema hayo wakati akikikabidhio kikundi cha Taifa cha Taarabu  na kusema wiraza yake imekitayarishia bajeti kikundi hicho kiliochosheheni waimbaji machachrii na wacharaza alla makini.

Amesema katika kuhakikisha kikindi hicho kinaimarika zaidi kitashirikishwa katika matamasha mbali mbali ya muziki ndani na nje ya nchi.katibu wa kikundi hicho pamoja na msanii Profesa Moh’d Iliyas wametowa shukrani kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweza kuwajali wasanii wa hapa nchini.

Mshauri wa Rais Sanaa na Utamaduni Chimbeni Kheri amesema wasanii wa kikundi cha taifa wanatoka katika vikundi mbali mbali hapa Zanzibar hivyo amewataka kuzidisha umoja na mashirikiano katika uwendeleza muziki wa taarab asili.

Naibu Katibu wa Wizara ya Vijana Sanaa,Utamaduni na Michezo Amour Hamil ameseama katika bajeti ya mwaka 2019/2020 watahakikisha wizara kukiendeleza zaidi kikundi hicho kwa kukipatia vyombo vya muziki .

Recent Comments by Fatma Muhamad

No comments by Fatma Muhamad yet.