Recent Posts by Fatma Muhamad

WANANCHI WAMETAKAIWA KUYALINDA MAENEO YA ASILI YA UZALISHAJI WA MAZAO YANAYOCHANGIA LISHE BORA

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi amesema wakati umefika kwa jamii kufikiria mbinu za kuyalinda maeneo ya asili yalioyokuwa vyanzo vya uzalishaji wa mazao yanayochangia lishe bora kwa Binaadamu.

Amesema zaidi ya maeneo 200 ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba tayari yameshavamiwa na maji ya Bahari kutokana na kuongezeka kwa harakati za kibinaadamu zilizopelekea uharibifu wa mazingira na matokeo yake kusita kwa shughuli za  uvuvi pamoja na kilimo.

Nd. Abdullah Hassan Mitawi amesema hayo wakati akiifunguwa Semina ya Siku Mbili inayohusiana na masuala ya Lishe inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Mtakwimu Mkuu wa Serikali liliopo Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Amesema ukataji ovyo wa Miti ya Mikoko sambamba na Uvunjaji wa Matumbawe umepelekea kuongezeka mara dufu kwa kiwango cha joto baharini na hatimae kusababisha upungufu wa samaki chakula kinachochangia lishe bora ambacho wakati mwengine hulazimika kuagizwa kutoka Nje ya Nchi.

Alitahadharisha kwamba matokeo ya upungufu wa lishe mwilini wakati mwengine hutokana na ukame baada ya kukumbwa na mabadiliko ya Tabia Nchi unaoweza kusababisha maafa kwa Wanaadamu.

Akitoa Mada Mtaalamu wa Masuala ya Lishe Nchini Tanzania Bwana Kavishe alisema Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba upungufu wa damu kwa akina Mama katika Visiwa vya Zanzibar umefikia asilimia 60% wakati upande wa  Watoto uko asilimia 65% kunakotokana na ukosefu wa virutubisho vya vyakula bora Mwilini.

Bwana Kavishe alisema Mkakati Maalum umeanzishwa Mwezi wa Agosti Mwaka 2018 katika kukabiliana na matatizo ya upungufu wa Lishe kwa baadhi ya Wananchi ambapo mapendekezo yake yameshawasilishwa Serikalini ili kupata baraka ya utekelezaji wake.

Hata hivyo Mtaalamu huyo wa masuala ya Lishe Nchini alishauri kwamba kufanikiwa na Mkakati huo kutatokana na ushiriki wa moja kwa moja wa Sekta zote kuanzia zile za Umma, Binafsi, Wananchi kwa kuunganisha na jitihada za Serikali Kuu.

Aidha Bwana Kavishe alieleza kwamba Mkatakati huo ni vyema ukajengewa utaratibu bora ya kufuatiliwa utekelezaji wake utakaokuwa ukionyesha matokeo yake kila baada ya kipindi.

 

MH. JOB NDUGAI AMERIDHISHWA NA HATUA ILIYOFIKIWA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi hasa katika kuimarisha huduma muhimu za jamii.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati akishiriki kazi ya ulazaji wa mabomba ya maji safi kutoka Bambi hadi Uroa na kuangalia maendeleo ya wakulima wa kilimo cha mpunga wa umwagiliaji maji katika bonde la Cheju kupitia mradi wa padep amesema Serikali ya Mapinduzi iko makini kusimamia miradi ya maendeleo ya wananchi jambo ambalo limeweza kuimarisha uchumi na kuwakwamua wananchi na umasikini.

Nae Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Dk Makame Ali Ussi amesema Serikali imekusudia kuendelea kuimarisha miundo mbinu ya umwagiliaji maji katika bonde la cheju ili wakulima walime kilimo chenye tija na kujitosheleza kwa chakula.

Afisa wa maji wilaya ya kati Ali Abdu Ali amesema mamlaka ya maji zawa imekuwa ikiendelea na juhudi mbali mbali za kuhakikisha wananchi wa kijiji cha Uroa wanapata huduma ya maji safi na salama katika kipindi kifupi kuanzia sasa.

TIMU YA JIMBO LA WETE IMEFANIKIWA KUTWAA UBINGWA WA MASHINDANO YA MAIDA CUP.

Timu ya jimbo la Wete imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindandano ya Maida Cupya kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwakwa CCM, baada ya kuitandika timu ya jimbo la Micheweni bao 2-1.

Mchezo huo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Konde Polisi, Jimbo la Wete iliyovalia jazi ya nja nailikuwa ya kwanza kulionalango la wapinzani wake kupitia kwa mchezaji Ali Mohamed kufunga mabao hayo katika dakika ya 22 na 49, huku Micheweni ikasawazishwa kupitia kwa Abdalla Khatib dakika ya 43.

Akizungunza na wanamichezo na washabiki, Mwenyekitiwa CCM Mkoawa Kaskazini Pemba, Mberwa Hamad Mberwa, amempongeza Mbunge  Maida kwa kuwaunga mkono vijana kupitia sekta ya michezo.

Mdhamini wa mashindano hayo na Mbunge wa kuteuliwa wa UWT Maida Hamad Abdalla, amesema mashindano hayo yamekusudia kutafuta vipaji vya wachezaji watakaounda timu ya Wilaya ya Wete na Mkoa.

Kwa  upande wa wanamichezo hao wamesem mashindano hayo yameamshaari katika timu zao.

Timu Wete imekabidhiwa shilingi laki mbili, kikombe, seti mbili za jezi, nishani na mipira mitatu, mshindiwa pili Micheweni ikipatiwa shilingi laki moja, jezi seti moja, mipira miwili na midali ya silva.

Huku zawadi mbalimbali zikitolewa ikiwemo kipa bora, mchezaji bora, mchezaji mwenye nidhamu, pamoja na timushiriki kila mmoja ikipatiwa mpira mmoja mmoja.

WANANCHI PUJINI WAMAETAKIWA KUTOA MASHIRIKIANO WAKATI WA UJENZI WA NGOME YA MKAMANDUME

Mkuu wa Wilaya ya ChakeChake Rashid Hadid Rashid amewataka wananchi wa Pujini wilaya ya Mkoani kutowa ushirikiano wakati wa ujenzi wa Ngome ya Mkamandume ili kufanikisha malengo ya serikali ya kurudisha haiba ya eneohilo.

Nd. Rashid ametowa wito huo kwenye mkutano wakukabidhi eneo la Mkamandume kwa Mkandarasi atakaejenga ngome hiyo Nd. Mansour Mohamed Kassim kutoka kampuni ya SHAMJO LTD.

Amesemaserikaliimekusudiakuliimarishaeneohilokwakurudishahistoriayakekubwaambayoinawavutiawagenikutokanchimbalimbaliduniani.

Akitowa maelezo ya eneo hilo Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Salum Kitwana Sururu na Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Khatib Juma Mjaja wamewasisitiza wananchi wa eneo hilo kudhibiti uharibifu na wizi katika kazihiyo.

Kwa upande wake Mkandari wa mradi wa ujenzi wa Ngome yaMkamandume Mansour Mohamed amesema watafanyakazi hiyo kwa kiwango kinachotakiwa na watawashirikisha wananchi katika harakati za ujenzi ili waanze kufaidika na Ngomehiyo.

Mradi wa ujenzi wa Ngome ya Mkamandume unakwenda sambamba na ujenzi wa gofu la Fukuchani Unguja ambayo kwa pamoja itagharimu kiasi cha shilingi milionimia 800.

Recent Comments by Fatma Muhamad

No comments by Fatma Muhamad yet.