Daily Archives: February 11, 2019

PBZ KUSHIRIKIANA NA USHIRIKA WA ELIMU SACOS

Benk ya watu wa zanzibar imesema iko tayari kushirikiana na ushirika la elimu sacos katika kufadhili miradi yake mikubwa ikiwemo ya ujenzi wa majengo ili kunoa sacos hiyo inafanikiwa katika malengo yake.

Imesema taasisi hiyo ya fedha  imeanzishwa kuwaendeleza kiuchumi wananchi kupitia miradi yao sambamba na kuchangia pato la taifa ili liwe imara zaidi katika kutoa huduma mbali mbali kwa wananchi hao.

Mkurugenzi mtendaji wa benk hiyo ndugu Juma Ameir ameeleza hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa kumi na nane wa elimu sacos uliofanyika katika viwanja vya aman mjini zanzibar na kufahamisha kwamba pbz kwa sasa iko vizuri zaidi kuwahudumia wateja wake.

Aidha amesema sambamba na kuwa tayari kushirikiana katika uanzishaji wa miradi mikubwa piaPBZ iko tayari kutoa mafunzo yanayohusu utunzaji wa fedha katika sacos hiyo.

Mwenyekiti wa sacos hiyo ndugu ahmed mohammed omar amesema sacos yake inatoa mikopo bila ya riba kwa wanachama wake na ina mtaji mkubwa kutokana na kuimarika kwake.

Katika risala ya wanasacos hiyo iliyosomwa na bi Halima Mohammed Issa imesema sacos inajitayarisha kujenga jingo la ghorofa litakalokuwa na maduka kama ni vitega uchumi vyake.