Monthly Archives: January 2019

KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA UHALIFU MAFUNZO YATOLEWA KWA VIKUNDI SHIRIKISHI

Naibu kamishna wa Polisi  Faustine  Shilogile ambaye ni  mkuu wa utawala wa rasilimali watu  wa -Polisi Zanzibar  amesema kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya  watu wamemua kutoa mafunzo kwa vikundi shirikishi katika shehia za wilaya ya mjini kwa lengo la kuondosha na kukomesha  vitendo hivyo.

Naibu kamishina Shilogile  ameyasema hayo Jango,mbe  matarumbeta wakati wa kufungua mafunzo kwa vikundi shirikishi  vya Wilaya ya mjini Magharib amesema mafunzo hayo yatasaidia kupambana  na kutokomeza vitendo vya uhalifu katika shehia zao

Amesema jeshi la Polisi limejipanga kutatua  matatizo yanayowakabili wanachi  kwa kuweka mikakati imara na kuwataka  wanachi kuwacha tabia ya  kujichukulia sheria mikononi mwao  baada ya kuwakamata wahalifu na badala yake kuwapeleka vituoni .

aidha imesema kazi ya ulinzi shirikishi  si ya jeshi  la Polisi pekee bali ni ya wote na kutoa tarifakwa lengo la kushirikiana pamoja.

Nae kaimu wa kamanda wa mkoa wa mjini PRC Saimon  Pasuwa  amewaopmba  vijana waliopewa mafunzo  hayo kuhakikisha  wanayatoa kwa wengine na kushirikiana pamoja kufichua wahalifu ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji wa jinsia kwa wanawake na watoto vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya watu.

MDC YAPINGA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA

Chama kikuu cha upinzani nchini zimbabwe mdc kimelaani vikali ukandamizwaji ulioshuhudiwa wakati wa kuzimwa kwa maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo. Kwa mujibu wa mashirika ya mawakili kwa ajili ya haki za binadamu yamebainisha kuwa zaidi ya watu 800 wamekamatwa wakiwemo wafuasi wa upinzani na wale wa mashirika ya kiraia. Katika mkutano na waandishi wa habari, chama kikuu cha upinzani cha movement for democratic change (mdc), kimelaani ukandamizaji wa siku za hivi karibuni nchini humo.  Hata hivyo serikali ya zimbabwe, inaushtumu upinzani kuandaa maandamano hayo na kuchochea vurugu.

 

WAMILIKI WA VYUO NA WADAU WA ELIMU ZANZIBAR WATKIWA KUFWATA TARATIBU ZA UDAHILI

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Mhe Riziki Pembe Juma amewataka wamiliki wa vyuo na wadau wa elimu zanzibar kuhakikisha kuwa udahili wanaofanya katika taasisi zao  unafuata utaratibu uliowekwa na baraza la elimu  ya sayansi na ufundi nacte

Akifungua  mkutano wa baraza hilo na wakuu wa vyuo mbalimbali wa taasisi za sayansi na ufundi   amesema kufuata utaratibu huo kutasaidia kuondosha tatizo la vyuo hewa na kupunguza wimbi la wahitimu wasio na sifa.

nae katibu mtendaji baraza la elimu ya sayansi na ufundi Dkt. Adolf Rutayuga amesema nacte inapaswa kuwafahamisha wakuu wa taasisi hizo  kufuata taratibu za usajili na pia kupitia mitaala yote ya vyuo hivyo ili kuondoa tatizo la wahitimu hewa.

Nao washiriki wa mkutano huo wameiomba nacte kuzidisha ushirikiano na taasisi hizo ili  kuondosha matatizo  baina ya wamiliki wa vyuo  na nacte.

BANDARI YA WETE NI MOJA YA BANDARI BUBU ZINAZOTUMIKA KUPITISHA BIDHAA HARAMU.

Mkuu wa wilaya ya wete Abeid Juma Ali amesema   licha ya wilaya hiyo kuwa na bandari kuu ya kusafirishia mizigo na raia  bado inakabiliwa na tatizo la bandari  bubu zinazotumika kupitisha bidhaa haramu.

Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama  ya wilaya hiyo, watendaji wa shirika la bandari pamoja na  wadau wa usafiri,  mkuu wa wilaya ya wete abeid juma ali  amesema baadhi ya wananchi hutumia mwanya wa uwepo na visiwa vidog vidogo, ikiwemo fundo, uvinje au kokota , kufanya udanganyifu  na kulishauri shirika la bandari kuandaa vitambulisho maalumu ambavyo vitatolewa kwa wananchi wanaokwenda katika visiwa hivyo.

Mkuu wa bandari ya wete Hassan Hamad Ali ,amesema  bandari hiyo inatumika kama njia ya kuingia na kutoka kwa watu kinyume nataratibu, na kuongeza baadhi ya bidhaa zinazotoka nje  kwa magendo  huhaulishhwa katika visiwa  vidog vidogo na kuingizwa kwa kutumia mashuwa kupitia bandari bubu.

Mwakilishi wa meli ya Sea Stars 1 Hassan Mohammed , amesema tangu meli hiyo ianze kuitumia bandari hiyo , wameweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza, ambapo mkuu wa wachukuzi bandarini hapo khatib hamad faki amesifu utaratibu uliowekwa na shirika la bandari.