Daily Archives: January 25, 2019

BARAZA LA SANAA SENSA NA FILAMU KUSIMAMIA VYEMA KAZI ZA SANAA.

Naibu waziri wa vijana utamaduni sanaa na michezo Mhe. Lulu Msham Khamis ameliagiza baraza la sanaa sensa na filamu kusimamia vyema kazi za sanaa.

Akifungua mkutano wa   kujadili kazi za sanaa    katika ukumbi wa wizara hiyo Mhe Lulu amesema baraza hilo linawajibu mkubwa wa kusimamia kazi za sanaa  hivyo amelitaka  kuonyesha michezo inayoendana na maadili, silka pamoja na desturi za wazanzibari.

mwenyekiti wa baraza la sanaa sensa ya filamu na utamaduni bibi  Maryam Mohd Hamdani amesema  katika kuzingatia  haki za wasanii wamekuwa wakiandaa matamasha  pamoja na kutoa mafunzo  ili  kuendeleza jitihada  za wasanii hapa nchini.

Katibu wa chama cha wasanii waigizaji zanzibar salum stika    amesema  chama cha wasanii na waigizaji  katika kuhakikisha hilo linafanikiwa  mwaka huu kimejipanga   kutengeneza filamu  zenye kukubalika  na kuwa na ubora  ili ziweze kuingia katika ulimwengu wa ushindani.

  

MPANGO MAALUM WA KUWEKA MIUNDOMBINU BORA YA USALAMA KWENYE VITUO VYA MAFUTA

Wamiliki wa vituo vya mafuta kisiwani pemba wametakiwa kuwa na mpango maalum wa kuweka miundombinu  bora ya usalama kwenye vituo hivyo ikiwemo kuwapa mafunzo wafanyakazi wao na kuweka vifaa vya huduma ya kwanza ili waweze kujiokoa panapotokezea matatizo.

Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na mkuu wa operation ya kukabiliana na maafa zanzibar Shaaban Hassan Ramadhan katika ziara ya ukaguzi wa bohari na vituo vya mafuta kisiwani humo

Amesema katika ukaguzi huo wamegundua mapungufu mengi ya kiusalama huku akitoa agizo la miezi mitatu kwa wamiliki kuyafanyia kazi mapungu hayo kabla ya kutokea maafa yasiyotarajiwa

Katika ziara hiyo mkuu wa operation ya uokozi kutoka kikosi cha zimamoto ali abdi hashim amesema baadhi ya vituo havina dawa mitungi ya kisasa ya kuzimia moto wala matangi ya maji hivyo kuwa vigumu kwao kuweza kujisaidia kunapotokea tatizo

Nao baadhi ya wasimamizi wa vituo hivyo vya mafuta wamesema watayafanyia kazi mapungufu madogo madogo yaliopo na yale makubwa watawasiliana na wamiliki wao kwa ajili ya kuyachukulia hatua

WANANCHI WA JIMBO LA JANG’OMBE WALIOJITOKEZA KUPIMA AFYA

Kati ya wananchi mia mbili na arobaini na tano wa jimbo la Jang'ombe na mitaa ya jirani waliojitokeza kupima afya kwa upande wa pressure jumla ya wananchi tisini na tatu  sawa na asilimia thelathini na nane wamegundulika kuwa na pressure ya juu ambayo ni hatarishi, baada ya kufanyiwa vipimo.

Hayo yameelezwa na mkuu wa kitengo cha maradhi yasiyo ambukiza ndugu Omar Mwalimu Omar mara baada ya kufanya tathmini ya zoezi la upimaji afyakatika kituo cha afya kiliopo urusi jimbo la jangombe, wilaya ya mjini.

Tathmini hiyo pia imeonyesha jumla ya watu 197 wamejitokeza kupima sukari na watu 22 sawa na silimia 11 wamegundulika kuwa na kiwango cha juu cha sukari, waliopima uzito ni 241 na watu 53 sawa na asilimia 22 wam3ebainika kuwa na  uzito uliopindukia.

Amesema waliogundulikana na matatio wamepewa ushauri wa kitaalamu kusudi kuendelea na matibabu na kama sio matibabukufuata njia sahihi ya kujiepusha na matatizo hayo

Mwakilishi wa jimbo la jangombe Mhe Ramadhani Hamza Chande amesema upimaji wa afya bure jimbo la jangome utakuwa endelevu na kutoa shukrani kwa mashirikiano na wananchi viongozi wa jimbo, manispaa na daktari dhamana.

Diwani wa wadi ya jangombe ndugu Saleh Fasihi amesema pamoja na huduma ya upimaji afya pia waliogundulika na kiwango cha juu cha sukari walipewa msaada wa lishe iliyokatika mchanganyiko maalum.

Mbali na upimaji pressure, sukari, uzito na urefu pia huduma ya upimaji macho na utowaji miwani bure kutoka hospitali ya macho mikunguniulifanyika kwa mafanikio makubwa.

 

 

SMZ ITAENDELEA KUTEKELEZA AZMA YA KUWAWEZESHA VIJANA

WAZIRI wa Kazi , Uwezeshji, Wazee, Wanawake na Watoto, Modiline Kastiko  amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar (smz) itaendelea kutekeleza azma  ya kuwawezesha vijana  ili kuweza kujiajiri katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji.

kauli hiyo ameitoa wakati akimwakilisha Makamu wa Pili wa Rais katika Uzinduzi wa Ushirika wa Ufugaji kuku kwa vijana wa Mkoa wa Mjini Magharib,

Mhe, Waziri Alisema miongoni mwa azma hizo ni kuhakikisha inatatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana kupitia wizara hiyo.

Ameongeza kuwa serikali imeona umuhimu wa kuanzisha wizara hiyo ili kuona vijana wanasaidiwa katika kuwatafutia mbinu mbalimbali za kuweza kijiajiri kwa lengo la kuondokana na vitendo viovu ambavyo vitawaharibia malengo yao ya maisha.

Waziri Castico amewataka vijana kuzitumia fursa hiyo ya mradi wa ufugaji kuku kwa lengo la  kujikwamua kiuchumi na  kuwawezesha vijana wengine kupata kuku hao na kuufanya mradi huo kuwa endelevu.

Castico amewataka vijana hao ambao wamepata mafunzo ya ufugaji wa kuku aina ya Saso kushirikiana na vijana wenzao kwa kuwapa elimu hiyo ili na wao waweze kufaidika na mardi huo na kuondokana na umasikini.

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo, Rashid Mohamed amesema kuanzishwa kwa ushirika huo wa vijana wa ufugaji kuku mkoa wa Mjini Magharibi una lengo la kuhakikisha vijana wanajiongezea kipato na endelevu.

Pia amiomba serikali ya SMZ kuongeza nafasi za ajira kwa vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwa kuendeleza taifa .

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmud, alisema mradi huo utawasaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kufikia uchumi wa kati.

"Mradii huu unatekelezwa kwa vitendo kwa kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe bila ya kutegemea ajira za serikali" alisema.