Daily Archives: January 24, 2019

KUNA HAJA YA WAFANYAKAZI KUPATIWA ELIMU ZAIDI KATIKA FANI TOFAUTI KWA MAENDELEO YA SHIRIKA

Mkurugezi  wa  Shirika  la utangazaji Zanzibar  Nd; Aiman Duwe  amesema ili shirika liwe  na  maendeleo na kuweza kuzalisha vipind tofauti kuna haja ya wafanyakazi kupatiwa elimu zaidi  katika fani tofauti kwa wafanyakazi hao.

Mkurugenzi  Aiman Duwe  ameeleza hayo alipokuwa katika kikao cha majibu ya hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali  kwa  mwaka wa fedha 2015/2016 kilichowajumuisha  wafanyakazi wa shirika la utangazaji zanzibar pamoja  na kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za  serikali na  mashirika[p.a.c]

Ndugu Aiman Duwe amesema  hadi sasa kuna baadhi ya wafanyakazi washapatiwa mafunzo na kwenda katika vyuo tofauti kwa  ajili ya kuongeza ujuzi zaidi na wakirudi anaimani shirika litazidi kupiga hatua na kuwa na muonekano mzuri kwa wananchi kwani hadi sasa tu wananchi wamekuwa wakilitumia kwa matangazo na habari mbali mbali.

Akielezea matumizi ya shirika la utangazaji amesema imeonekana kuongezeka  kutoka shiling  bilioni sita kwa mwaka wa fedha 2015/2016 na kuwasisitiza wafanyakazi wa shirika hilo kuzidisha mashirikiano katika kazi ili shirika liweze kuongezeka zaidiii …

Nae makamo mwenyekiti wa [p.a.c] Mh; Shaibu said  amesema lengo kubwa la kufika katika shirika la utangazaji zanzibar ni moja ya kutimiza majukumu ya kiutumishi ya kutizama Hisabu ya matumizi na mapato ya hesabu za serikali na si Wizara hiyo tu bali ni Wizara zote  na kumpongeza mkurugenzi huyo kwa hatua aliyofikia..

 

MH SAMIA SULUHU HASSAN AMEWATAKA WANAWAKE NCHINI KUTOKUWA NA WOGA NA KUJIAMINI

Makamo wa raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mh Samia Suluhu Hassan  amewataka wanawake nchini kutokuwa na woga  na kujiamini   katika kudai haki zao za msingi pale wanapoona zinavunjwa.

Amewataka wanawake kujitokeza  kujiingiza katika  nafasi za uongozi  za  mahakama  ili kupatikane haki na usawa   katika vyommbo vya    kisheria.

akifungua   mkutano wa tisa wa  chama cha majaji wanawake tanzania   (TAJWA)    uliofanyika  hoteli  verde mtoni mh samia  amesema   chama  hicho ni chombo muhimu  nchini  katika  mahakama kuu  kutokana  na kutoa fursa   za uendeshaji wa kesi za wanawake   ambazo huingizwa   katika mkondo wa kisheria .

Amesema katika uchumi wa viwanda ushiriki wa wanawake waliowengi unaonekana kuwa mdogo  katika sehemu zao za kazi  hivyo mh samia  ame kitaka      chama cha TAJWA kuhakikisha  wanawake wanawashirikisha   vyema katika uchumi wa  aina hiyo  ambao   ndio  kauli mbiu  katika mkutano huo  wa siku mbili wa mwaka huu.                                              

jaji mkuu  tanzania Profesa Ibrahim Juma  amesema  kuwepo kwa   chama cha majaji wanawake tanzania  kunaisadia mahakama  kuwa na chombo kinachohakikisha usawa wa wanawake   na  kuielimisha jamii   katika kuhakikisha kunakuwa na usawa wa jinsia  ya aina hiyo.

mwenyekiti wa chama  cha majaji wanawake tanzania Jaji Iman Aboud  amesema   mkutano huo     u naangalia ukuaji wa viwanda hapa nchini bila ya kuwabaguwa wanawake katika  ushiriki  wao , sheria na taratibu pamoja na nafasi za kupatiwa mikopo  bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Mkutano huo  wa tisa umewakutanisha majaji  pamoja na mahakimu wa mikoa na wilaya.

WAKULIMA WA MWANI WA KIJIJI CHA PAJE WAPATA KHOFU JUU YA KILIMO CHAO

Wakulima wa mwani wa kijiji cha paje wameuomba uongozi wa wizara ya kilimo kupitia idara ya maendeleo ya uvuvi kuangalia harakati za watalii za michezo ya baharini katika fukwe za paje kwani zimeanza kuwajengea hofu juu ya kilimo chao cha mwani.

Wakulima hao wameiambia ZBC kuwa watalii wanafanya   michezo ya maputo smoklin karibu na maeneo ya fukwe wakati ambapo kilimo cha mwani kikiwa kinaendelea.

Wamesema kuwa ingawa utalii una faida sana katika taifa  lakini ni vyema taasisi husika zikakaa pamoja kuwapangia maeneo maalum ambayo wao watafanya michezo yao hiyo  na harakati za kilimo cha mwani zikiendelea.

Akilitolea ufafanuzi suala hilo mkurugenzi idara ya maendeleo ya uvuvi Nd Mussa Aboud Jumbe amesema watakaa pamoja na mamlaka ya uwekezaji ili kutafuta muafaka wa tatizo hilo bila ya kutokea athari yoyote.

(COSOZA) NA (NCAC) WAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SANAA PAMOJA NA KUBADILISHANA UZOEFU.

Afisi ya hakimiliki zanzibar (COSOZA) imesema mashirikiano waliyoanzisha baina yao na taasisi ya hakimiliki ya jamhuri ya watu wa china (NCAC) itasaidia kuimarisha ushiriakiano katika sanaa pamoja na kubadilishana uzoefu.

hayo yameelezwa na naibu katibu mkuu wizara ya vijana ,utamaduni ,sanaa na michezo Amour Hamili Bakari katika mkutano wa mashirikiano baina ya ofisi ya hakimiliki ya zanzibar na ofisi ya hakimiliki ya jamhuri ya watu wa china uliofanyika mazizini.

amesema pamoja na mashirikiano hayo pia ushirikiano huo utasaidia kutoa fursa kukabiliana na wizi wa kazi za sanaa

katibu mkuu wa  hakimiliki   zanzibar ( COSOZA) mtumwa ameir khatib amesema  taasisi ya hakimiliki ya china iko juu katika teknolojia  hivyo itasaidia zanzibar kuwa na mbinu madhubuti  za kupambana na uharamia wa kazi za wasanii hasa katika mitandao ya kijamii.

katibu wa chama cha wasanii na waigizaji zanzibar salum maulid amesema huu ni mwanzo mzuri kwa wasanii wa zanzibar kwani itasaidia kufungua milango na kukuza sana ya zanzibar kutokana na sanaa ya china kukua zaidi ukilinganisha na ya zanzibar

nae mkurugenzi mkuu wa taasisi ya hakimiliki ya china NCAC tang zhaozhi amesema ushirikiano huo ni muhimu baina ya nchi mbili hizi kwani utasaidia kulinda haki za wasanii ndani na nje ya Nchi.