Daily Archives: January 23, 2019

MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATAKIWA KUFANYA UTAFITI WA KUTOSHA KABLA YA KUTOA VIPIMO KWA WANANCHI

Waziri wa afya Mhe Hamad Rashida Mohamed ameitaka bodi ushauri  na wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kutoa vipimo kwa wananchi ili kuepuka mifarakano katika jamii.

Hayo ameleza wakati akizidua bodi mpya  ambapo alitaka kutoa  elimu zaidi kwa wananchi pamoja na maskuli jinsi ya matumizi ya  kipimo cha DNA kwani wananchi walio wengi hawajuwi jinsi ya kipimo hicho kinavyo tumika.

Aidha alitaka  bodi hiyo kuvitunza vifaa hivyo muhimu ambavyo vimegharimu fedha nyingi ili viweze kudumu kwa muda mrefu kwa maslahi ya nchi na wananchi.

Mwenyekti  bodi hiyo Haji Mwamvura Haji amesema bodi hiyo itajikita zaid katika kufanya utafiti pamajia na kuwa wabunifu ili kuhakikisha kuwa lengo lilokusudiwa linanapatika  na kuhakikisha kuwa majibu yanayotolewa katika maabra yanakuna ni sahihi.

Nae mwenyekiti mstaafu wa bodi hiyo aliemaliza muda wake alishukuru mashirikiano aliyoyapata katika kufanya kazi zake na kuitaka bodi hiyo mpya kukaa pamoja na taasisi zinazohusiana na mambo ya sayansi ili kuweza kufanya kazi zao kwa uhakika zaidi.

WANAMUZIKI ZANZIBAR WAMETAKIWA KUTUNGA NYIMBO ZA KUELIMISHA JAMII

Wanamuziki zanzibar wametakiwa kutunga nyimbo za kuelimisha jamii katika mambo mabil mbali yanaotokezea pamoja na kuitumia studio za musiki ya rahaleo iliyojengwa kwa harama kwa kuwasaidi wasanii na kukuza vipaji.

Akizungumza na kamati ya baraza la wakilishi ilipokwenda kuangalia maendeleo ya mafanikio ya studio maendeleo ya wanawake, habari na utalii meneja wa studio hiyo Abeid Mfaume amesema studio hiyo ni ya kisasa na pia ina sifa zote zinazo stahili amewataka wananchi kujitokeza kupeleka kazi zao.

Kwa upande wa rais wa wasani Mohd Abdallah  ametolea ufafanuzi wa juu ya wasanii amesema changamoto kubwa wanazozipata ni juu ya mashairi yasiyo na maadili ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wasanii kutojitokeza kutumia studio hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya habari,maendeleo,wamnawake na utalii Mwantatu Mbarak Khamisi  amepata fursa ya kuweza kurekodi studio hiyo.

 

 

 

VYUO VYA MAFUNZO ZANZIBAR VYAEKA UTARATIBU MAALUMU WA KUENDELEZA KILIMO

Uongozi wa vyuo vya mafunzo zanzibar , umesema uweka utaratibu maalumu wa kuendeleza kilimo, ili kuwafanya wanafunzi wa vyuo vya mafunzo kuwa wazalishaji wanapomaliza muda wa kutumikia vyuo hivyo.

Hayo yamesema na Kamishna wa vyuo vya Mafunzo Zanzibar Ali Abdalla wakaati wa zoezi la uzinduzi wa uvunaji wa mpunga katika kambi ya chuo cha Mafunzo Tungamaa Wilaya ya Wete.

Aidha Kamishna Ali Abdalla amesema zoezi hilo la uvunaji wa Mpunga katika mabonde ya Tungamaa , umelenga kuongeza uzalishaji wa chakula kwa wanafunzi wa vyuo vya mafunzo.

Naye Mkuu wa kambi la chuo cha Mafunzo Tungamaa, Mkaguzi Hafidh Haji Mcha, amemshukuru kamishna kwa uwamuzi wake wa kushiriki zoezi la uvunaji wa Mpunga katika bonde la Tungamaa.

Mkaguzi Hafidh , amesema zoezi hilo la uvunaji wa Mpunga ni kuunga mkono mapinduzi ya Zanzibar ya januari , 1964.

Wananchi wamezoea kuona viongozi wanazindua majengo,barabara na huduma nyengine , lakini uwamuzi wa kamishna anaunga mkono.

Kamanda Haji amewataka wananchi kushirikiana na askari wa vyuo vya mafunzo katika kuimarisha sekta ya kilimo kwa wanafunzi.

Imekuwa ni kawaida wa askari wa vyuo vya mafunzo kuwashirikisha viongozi kwa ajili ya kuvuna mpunga ambapo msimu uliopita zoezi hilo lilizinduliwa na Mhe Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman.