Daily Archives: January 22, 2019

BARAZA LA MAWAZIRI LARIDHIA UTOZWAJI WA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT) KWA 0%

Baraza la mawaziri limeridhia utozwaji wa kodi ya ongezeko la thamani (vat) kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye umeme unaouzwa na shirika la umeme tanzania (tanesco) kwa shirika la umeme la zanzibar (zeco) na kufuatia malimbikizo ya deni la kodi ya vat liliofikia shilingi bilioni 22.9 kwa tanesco kwenye umeme uliozwa zeco.

WIZARA YA VIJANA ,UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO YAUNGA MKONO JITIHADA ZA VIJANA

Wizara ya vijana ,utamaduni  sanaa na michezo imesema itaendelea kuunga mkono jitihada za vijana katika kuanzisha miradi inayoanzishwa na vijana hao ili waweze kupata ajira.

akifungua kikao  cha utekelezaji mwenyekiti  wa baraza la vijana Ndugu Khamis Hassan Kheir amesema kikao hicho kimejadili utekelezaji wa mazimio waliyoyapitishajuu ya kuanzishwa miradi ya kilimo cha hema kwa vijana katika maeneo mbali mbali ya wilaya.

Afisa mipango wa baraza  hilo Ndugu Kheir Hassan Khamis amesema endapo vijana watajituma  na kulima  kilimo cha kisasa na kuacha kutumia  kilimo cha kemikali  wanaweza kuhamasisha vijana wengine  kufanya shughuli za kujipatia kipato  cha taifa na kupiga hatua kubwa za maendeleo Nchini.