Daily Archives: January 21, 2019

WADAU WA MICHEZO WAJITOKEZA KUSAIDIA KLABU YA KIKWAJUNI

Wadau wamichezo wajitokeza kuisaidi klabu ya kikwajuni na kutoa ahadi ya kuisaidi klbu hiyo kurudisha makali yake kama zamani.

Akizungumza na wanachama wa klabu hiyo mdau wa michezo Mohd Raza amesema klabu hiyo watahakikisha inakuwa katika hadhi yake kwa kuisaidi na kuiwezesha kwa nyezo mbali mbali za kimichezo.

Mwenyekiti wa klabu ya kikwajuni kocha buruhani msoma pamoja na kocha wa zamanim wa timu hiyo Ibrahi  Raza wamesema mashirikiano ndio ngao ya kuiwezesha timu hiyo kurudi katika makali yake.

 

EREA KUJADILI MASUALA YA NISHATI YA NCHI ZAO

Umoja wa wadhibiti wa mambo ya nishati Afrika mashariki erea umeanza mkutano wake hapa Zanzibar kujadili masuala ya nishati ya nchi zao hasa kutokana na kuongezeka kwa mabadiliko ya tabia nchi katika nchi hizo.

Mkurugenzi wa gesi  asilia ewura tanzania Ndugu Cherles Umujuni amewaambia wandishi wa habari kwamba mkutano huo unazishirikisha mamlaka za udhibiti wa nishati hiyo za nchi wanachama  wa umoja huo ambao ni Burundi, Rwanda,  Uganda, Kenya,  Tanzania na wenyeji Zanzibar.

Mkuu wa  kitengo cha uhusiano cha mamlaka ya  huduma za maji  na nishati zanzibar zura Khuzaima Ali  Bakar  amesema mkutano huo  mbali ya kuzungumzia masuala ya nishati ya mafuta lakini pia  utazungumzia masuala ya umeme, hali ya uchumi pamoja na masuala ya kisheria yanayohusu nishati hiyo.

DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA NIGERIA DKT. OLUSEGUN OBASANJO

Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na rais mstaafu wa nigeria Dkt. Olusegun Obasanjo ikulu jijini dar es salaam.

Katika  mazungumzo hayo Dkt. Obasanjo amempongeza Mhe. Rais magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya katika uongozi wake ikiwemo kupambana na rushwa, kuimarisha utoaji wa elimu, kuimarisha miundombinu, kuongeza nishati ya umeme, kuimarisha usafiri wa ardhini na angani na jinsi wadau mbalimbali wa ndani na nje wanavyopaswa kuelewa juhudi zinazofanyika.

Dkt. Obasanjo amesema Mhe. Rais magufuli amedhihirisha kuwa kiongozi imara wa kusimamia mambo muhimu yenye maslahi kwa nchi yake na amebainisha kuwa licha ya kwamba maendeleo ya nchi hayapatikani mara moja lakini kwa muda mfupi Mhe. Rais magufuli amefanya juhudi kubwa za kuimarisha maeneo ya huduma za kijamii, kukiimarisha chama chake cha siasa.

Mapema  Mh. Rais magufuli amepokea hati za utambulisho za mabalozi watatu walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao  baada ya waliokuwa mabalozi wa nchi hizo kumaliza muda wao.

Waliwasilisha hati ni balozi wa jamhuri ya korea hapa nchini Mhe. Cho tae-ics, balozi wa malawi hapa nchini mhe. Glad chembe munthali, na balozi wa brazil hapa nchini mhe. Antonio augusto martins cesar