Monthly Archives: December 2018

WATENDAJI WA SEKTA YA AFYA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KUWA WAZALENDO

Mkurugenzi wa  halmashauri ya wilaya ya Kaskazini “A” Nd: Mussa Ali Makame  na mwenyekiti wa  halmashauri hiyo Nd: Hassan Mcha Hasan wamewataka watendaji wa sekta ya afya katika halmashauri hiyo kufanya kazi kwa bidii kwa kuweka uzalendo mbele pamoja na kufuata miongozo na sheria za utumishi wa umma ili kuleta huduma zilizo bora kwa wananchi.

Wakizungumza katika kikao kilichojumuisha uongozi wa halmashauri pamoja na watendaji wa sekta ya afya katika ofisi ya halmashauri mkokotoni wamesema utendaji kazi wa sekta hiyo bado upo chini ukilinganisha na kasi ya maendeleo ya halmashauri hiyo hivyo ni wajibu wa wafanyakazi hao kuwa wazalendo katika kazi zao ili kuepuka malalamiko ya wananchi .

Nao watumishi wa sekta hiyo wamesema changamoto zilizopo hivi sasa ni ukosefu wa maji kwa baadhi ya vituo vya afya, usafiri kwa wafanyakazi pamoja na baadhi ya viongozi kuwa sio wataalamu wa afya jambo ambalo linasababisha wao kuonekana wanakwenda kinyume na utendaji wa kazi.

Kwa upande wake afisa muendeshaji wa halmashauri hiyo nd: fakihi kombo faki  amesema halmashauri tayari wameshaanza kuzitatua changamoto za watendaji wa halmashuri hiyo ikiwemo changamoto ya maji kwa baadhi ya vituo vya afya .

Katika kikao hicho mada mbili zilijadiliwa ikiwemo utambuzi wa muundo na kazi za halmashuri pamoja na maadili katika utumishi wa umma.

ZU KUELEKEA DODOMA KWENYE MASHINDANO YA VYUO VIKUU VYA AFRIKA MASHARIKI (TUSA).

Timu ya zanzibar university imeondoka zanzibar kuelekea dodoma kwenye mashindano ya vyuo vikuu vya afrika mashariki (TUSA). Jumla ya msafara wa wanafunzi 25 na viongozi watano wa mabingwa ya soka ya vyuo vikuu tanzania ambao pia ni makamo bingwa wa vyuo vikuu vya Africa mashariki (TUSA) timu ya zanzibar university(ZU) wameondoka leo kutoka zanzibar kwenda dodoma kwa ajili ya  mashindano ya vyuo vikuu vya afrika mashariki.

Akizungumza wakati anaondoka bandarini malindi mjini unguja kocha msaidizi wa timu hiyo , Nd Hussein Suleiman Ali amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanarudi na kombe hilo.

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo ndugu Haji Ramadhan amesema kasi itakuwa ndio ileile, huku akiwatoa khofu wazanzibar na watanzania kwenye mashindano hayo.

Mashindano hayo yanategemea kuzinduliwa jumatatu december 17 maeneo ya chuo kikuu cha dodoma (UDOM) na Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania MHE Kassim Majaaliwa ambapo zaidi ya vyuo 50 vikitarajiwa kushiriki ambapo vyuo 17 kutoka Tanzania, 17 vya Kenya , 18 vya Uganda, vitatu vya Burundi huku Ruwanda na wageni waalikwa Zambia wakitoa mshiriki mmoja mmoja.

DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMEIPONGEZA MISRI KWA KUENDELEA KUWA KICHOCHEO CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI

Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli  ameipongeza misri kwa kuendelea kuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi kwa nchi za kiafrika.

Ikulu jijini dar-es-salaam rais magufuli ameyasema hayo baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa maporomoko katika mto rufiji, mkataba uliohusisha kampuni ya ukandarasi ya arab contractor ya nchini misri na shirika la umeme tanesco na kushuhudia pia na waziri mkuu wa misri mhe dkt mostafa madbouly.

Amesema nchi ya misri itakumbukwa kwa mchango wake wa dhati kwani kutokana na uhusiano wake na tanzania ulioasisiwa na rais wa kwanza wa tanzania hayati mwalimu julius nyerere na rais wa kwanza wa misri gamal abel nasa ulikuwa ni chachu ya kuanzisha umoja wa nchi huru za kiafrika na harakati za ukombozi.

Rais magufuli akawataka watanzania kuunga mkono mradi huo  ambao hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi za kitanzania trilioni 6.558 kwani utachangia mabadiliko ya kiuchumi kutokana nakushuka kwa bei ya umeme na hivyo kuleta tija kwa uzalishaji wa kiviwanda na kumudu ushindani wa kimasoko.

Naye waziri mkuu wa jamhuri ya kiarabu ya misri mhe mostafa madbouly amesema  katika kuendeleza uhusiano wa misri na tanzania  tayari makampni kadhaa ya nchini misri yameitikia mwito wa kufanya shughuli zao nchini tanzania.

Waziri wa madini mhe dkt medadi kalimani amesema kukamilika kwa mradi huo kutaifanya tanzania kufikia azima yake ya kuwa nchi ya viwanda na ya uchumi wa kati, na bwawa la mradi huo ni miongoni mwa mabwawa 70  dunia ambapo kwa ukubwa linashika nafasi ya sitini kidunia, na ni la nne kwa afrika huku likisha nafasi ya kwanza kwa afrika ya mashariki.

Naye waziri wa nishati wa misri mohamed shapa amesema kukamilika kwa mradi huo kutaiwezesha tanzania kuingia katika mapinduzi ya viwanda.

UJIO WA MELI MPYA YA SEA STAR 1 KATIKA BANDARI YA ZANZIBAR

Ujio wa meli ya sea star 1 katika bandari ya zanzibar itapelekea kupunguza changamoto zilizokuwepo kwa wananchi wanaosafiri kutoka zanzibar, tanzania bara na tanga kwa kuweza kuwarahisishia.

Kepteni wa meli hiyo, Nasour Abubakari, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na zbc  baada ya ukaguzi wa meli hiyo ilipowasili zanzibar huko katika gati ya malindi mjini unguja.

Aidha amesema madhumini hasa ni kuweza kuunganisha kiusafiri kwa wananchi pamoja na kuwapunguzia harama na kuwapa urahisi kwa kila mwananchi.

Nae mfanyabiashara ambae ni mmiliki wa meli hiyo, salim turki, amesema nia na ndoto ya kuletwa meli hiyo ambapo itaweza kuwasaidia wananchi. Hivyo ameahidi kufanya kazi kama walivyomueleza ili kuona wananchi kuona jihudi na serikali kutatua tatizo kwa wananchi linafikiwa pamoja na wananchi kukitumia chombo hicho kitakapoanza kufanya kazi.

Naodha  mariya pamoja na msaidizi wake ambaye aliyekifikisha chombo hicho hapa nchini kutokea ugiriki amesema chombo hicho ni kimpya na kimetengenezwa nchini ugiriki mwaka 2018,ambapo kimechukua takribani siku 19 hadi kufika zanzibar.

Amesema chombo kimekuwa na ubora wa hali ya juu ambapo chombo hicho kimekuwa na ubora zaidi na kinaweza kuchukua abiria zaidi ya wananchi 1000, gari 200.